CHADEMA WAVURUGANA SHINYANGA …KATIBU MWENEZI CHADEMA ATUMBULIWA KUZUIA MKUTANO WA CHADEMA POLISI..MWENYEWE AKAZA

Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA
mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akiwataarifu wanachama wa Chadema juu
ya mkutano wao kuzuiwa kufanyika baada ya Katibu Mwenezi wa Chadema
Wilaya ya Shinyanga Mjini,Charles Shigino kuandika barua jeshi la polisi
kuwa kuna taarifa za uvunjivu wa amani kwenye mkutano wa Chadema. 
Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Baraza la Uongozi la Chama Cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) mkoa wa Shinyanga limemsimamisha
nafasi zote za uongozi Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga
Mjini, Charles Shigino kutokana na kwenda kinyume cha Katiba ya Chama,
Kanuni na Maadili ya Viongozi wa Chama kwa kuzuia mkutano mkuu wa
CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini kwa kuandika barua Jeshi la Polisi
akidai kuna dalili za uvunjifu wa amani endapo mkutano ungefanyika.Akizungumza na Vyombo vya Habari leo
Jumanne Januari 21,2020 katika ofisi za CHADEMA wilaya ya Shinyanga
Mjini,Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga,
Emmanuel Ntobi amesema Baraza la Uongozi CHADEMA limechukua hatua hiyo
baada ya kukutana katika kikao cha dharura cha kamati tendaji na kubaini
kuwa Shigino amekiuka katiba ya chama na kanuni na taratibu za uongozi.“Baraza limemsimamisha nafasi zote za
Uongozi ndani ya Chama,Ndugu Charles Shigino ambaye alikuwa Katibu
Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini na Mjumbe wa mkutano mkuu
kata ya Ngokolo. Atabaki kuwa mwanachama na tunamuandikia barua ajieleze
ndani ya siku 14 kwa nini asifukuzwe uongozi”
,amesema Ntobi.“Tulikuwa na mkutano mkuu wa
wanachama wa Jimbo la Shinyanga Mjini leo katika ukumbi wa Ibanza
Hoteli,tumeshangaa kupata taarifa kuwa Jeshi la polisi kupitia kwa mkuu
wa polisi wilaya ya Shinyanga kuwa mkutano wetu umezuiwa kufanyika
kutokana na barua iliyoandikwa na Shigino aliyeomba polisi wazuie
mkutano kwamba kuna hatari na uvunjifu wa amani”,
ameeleza Ntobi.Amesema kutokana na hali hiyo viongozi
wa CHADEMA walifika katika kituo cha polisi wilaya ya Shinyanga na
kukutana na mkuu wa polisi wilaya (OCD) ambaye aliwaeleza kuwa wamezuia
mkutano huo kutokana na barua ya mwenzao na ndipo Kamati tendaji ya
Chadema ilipokaa katika kikao cha dharura na baraza la uongozi kuchukua
uamuzi wa kumchukulia hatua Shigino.“Shigino amekiuka maadili ya
uongozi,amefanya utovu wa nidhamu,amekisaliti chama na kupanga njama ya
kuhujumu chama na kutoheshimu ngazi za juu za uongozi katika chama.
Shigino amekuwa na tabia ya kupinga maamuzi ya viongozi wenzake katika
chama”
,amesema Ntobi.


“Kwa mujibu wa Katiba ya CHADEMA ya
Mwaka 2006, Toleo la 2016. Ibara ya 7.5.4 (h) Baraza la Uongozi Mkoa,
ndio Mamlaka ya nidhamu na uwajibishaji wa Viongozi wa Jimbo/Wilaya.
(Ibara ya 6.3.6(iv).Kwa maana hiyo, Baraza la Uongozi limechukua hatua
za kinidhamu dhidi yake, kwa kuzingatia Ibara ya 6.3.6.(d).Hivyo, kuanzia leo, tarehe
21.01.2020, Chama kinatoa taarifa kwa umma na Wanachama kuwa Charles
Shigino, amesimamishwa  ukatibu mwenezi wa Jimbo la Shinyanga Mjini
mpaka hapo itavyoamuliwa vinginevyo”,
amefafanua.Ntobi amebainisha kuwa mkutano huo mkuu
wa wanachama ulilenga kujadili masuala mbalimbali ya kujenga CHADEMA
ikiwemo kuwapa wanachama muhtasari wa mambo yaliyojiri katika Mkutano
mkuu wa CHADEMA taifa uliofanyika hivi karibuni na kujadili waraka wa
Katibu mkuu wa CHADEMA.Naye Katibu wa Baraza la Uongozi CHADEMA
Mkoa wa Shinyanga, Zacharia Obad amesema Shigino anayo nafasi ya
kujitetea ndani ya siku 14 na kukata rufaa baada ya siku 30 kuhusu
maamuzi yaliyochukuliwa na Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa.Aidha amesema CHADEMA haitasita kuwachukulia hatua wale wote wanaokwenda kinyume na maadili na katiba ya CHADEMA.

Hata hivyo Shigino akizungumza na
Malunde 1 blog amesema kitendo cha kuweka zuio la mkutano wa wilaya ya
Shinyanga Mjini kutokana na kwamba viongozi wa Baraza la Uongozi CHADEMA
mkoa wa Shinyanga limekiuka katiba ya Chadema kwa kuitisha mkutano
mkuu wa wilaya ambao hawastahili kuuitisha na kuhudhuria labda kama
watakuwa wamepewa mualiko wa wageni waalikwa tu.

Shigino amesema kutokana kutoelewana
kwake na viongozi wa baraza la uongozi Chadema mkoa wa Shinyanga kuhusu
mkutano huo ndiyo kumemfanya aweke zuio kwa kutumia jeshi la polisi
kwani hali isingekuwa shwari ndani ya mkutano huo.

“Ni kweli nimeweka zuio la mkutano wa
Chadema kuzuia viongozi hawa waliokanyaga katiba ya CHADEMA. Mkutano
wao ulikuwa Batili,Wametumia katiba gani hawa viongozi wa mkoa ambao ni
viongozi wa baraza la uongozi wa mkoa na vikao vya mashauriano tu
kuitisha mkutano wa wilaya halafu wao ndiyo wakawe wageni rasmi na
wasemaji kwenye Mkutano mkuu wa wilaya. Kwenye mkutano huo pia waliita
waliokuwa wagombea uenyekiti serikali za mitaa kuhudhuria mkutano..Sasa
hapa wametumia katiba gani?,
amehoji Shigino.

“Bado sijapata barua ya kusimamishwa
uongozi. Lakini hawa Viongozi wa baraza la uongozi Chadema mkoa siyo
wajumbe wa mkutano mkuu wa wilaya, Wamepata wapi haya mamlaka
?.Nitaripoti kwa viongozi wa Kanda ya Serengeti kilichotokea. Nataka
nijue nani anatakiwa kutumbuliwa kati yangu na wao ambao wamekanyaga
katiba?”
,amesema.

Hata hivyo Shigino amesema yeye bado ni
mwanachama wa CHADEMA na atabaki kuwa CHADEMA na ataendelea kuwa katibu
Mwenezi Wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini na hapendi kuona Chama
kinaharibiwa na watu wachache vimelea wanaotengeneza fitna ambao
wanashiriki kuleta vurugu ndani ya chama.

Shigino alihamia CHADEMA mwaka 2015
akitokea CCM akiwa Katibu Mwenezi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini na
Januari 15,2019 alichaguliwa kuwa Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya
Shinyanga Mjini.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Hapa ni nje ya ofisi za Chadema wilaya
ya Shinyanga Mjini,Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa
Shinyanga, Emmanuel Ntobi akiwataarifu wanachama wa Chadema juu ya
mkutano wao kuzuiwa kufanyika baada ya Katibu Mwenezi wa Chadema Wilaya
ya Shinyanga Mjini,Charles Shigino kuandika barua jeshi la polisi kuwa
kuna taarifa za uvunjivu wa amani kwenye mkutano wa Chadema uliotakiwa
kufanyika leo Januari 21,2020 katika ukumbi wa Ibanza Hoteli Mjini
Shinyanga. Picha zote na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA
mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akitoa taarifa kwa wanachama wa
Chadema kuhusu hatua iliyochukuliwa na Baraza la Uongozi Chadema mkoa
kumsimamisha nafasi zote za uongozi Charles Shigino.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA
mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akitoa taarifa kwa wanachama wa
Chadema kuhusu hatua iliyochukuliwa na Baraza la Uongozi Chadema mkoa
kumsimamisha nafasi zote za uongozi Charles Shigino.
Wanachama wa Chadema wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA
mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akisoma katiba ya Chadema na vifungu
alivyokiuka Shigino.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA
mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akizungumza na waandishi wa habari
ndani ya Ofisi ya CHADEMA Shinyanga Mjini leo Januari 21,2020 na kuwapa
taarifa ya kumsimamisha 
nafasi zote za uongozi Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Shigino.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA
mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akizungumza na waandishi wa habari
ndani ya Ofisi ya CHADEMA Shinyanga Mjini leo Januari 21,2020 na kuwapa
taarifa ya kumsimamisha 
nafasi
zote za uongozi Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini,
Charles Shigino.Kushoto ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake Chadema mkoa
wa Shinyanga Winfrida Mwenula. Wa kwanza kulia ni  Mwenyekiti wa 
Madiwani wa CHADEMA mkoa wa Shinyanga ,William Shayo akifuatiwa na
Katibu wa 
Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga,Zacharia Obad.
Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi CHADEMA
mkoa wa Shinyanga, Emmanuel Ntobi akionesha barua ya Charles Shigino
kuzuia mkutano wa wanachama wa CHADEMA.
Katibu wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga,Zacharia Obad akielezea zaidi kuhusu maamuzi waliyochukua dhidi ya Charles Shigino.
Katibu wa Baraza la Uongozi CHADEMA mkoa wa Shinyanga,Zacharia Obad akielezea zaidi kuhusu maamuzi waliyochukua dhidi ya Charles Shigino.
Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya
Shinyanga Mjini, Charles Shigino naye akizungumza na waandishi wa habari
dhidi ya maamuzi ya 
Baraza la
Uongozi la CHADEMA mkoa wa Shinyanga kumsimamisha nafasi ya Katibu
Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo amesema maamuzi hayo
ni batili na ataendelea na nafasi hiyo na kubaki kuwa mwanachama
mwadilifu wa Chadema.
 
Katibu Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya
Shinyanga Mjini, Charles Shigino naye akizungumza na waandishi wa habari
dhidi ya maamuzi ya 
Baraza la
Uongozi la CHADEMA mkoa wa Shinyanga kumsimamisha nafasi ya Katibu
Mwenezi wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo amesema maamuzi hayo
ni batili na ataendelea na nafasi hiyo na kubaki kuwa mwanachama
mwadilifu wa Chadema.
 
Picha zote na Kadama Malunde – Malunde  1 blog