CHADEMA ZANZIBAR CHADAI MWITIKIO WA WANACHAMA KUCHUKUA FOMU NI KUBWA

Mbowe released after 8 hours of grilling - The Citizen

Na Thabit Madai ,Matukiodaima Zanzibar

 CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Kanda ya Unguja kimesema kwamba Muitikio ni mkubwa kwa Wananchama wa Chama hicho katika kujitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa kwa chama kuchaguwa kuwa wagombea wa nafasi za uwakilishi na ubunge katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi oktoba mwaka huu.

 Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa chama chama hicho kanda ya Unguja, Said Mzee Said wakati akizungumza na waandishi wa Habari katika Ofisi kuu za chama hicho zilizopo kisiwandui Mjini Unguja.

 Said Mzee Said alisema kwamba mchakato wa Uchukuaji wa fomu kwa nafasi ya uwakilishi na ubunge ulianza Julai 04 hadi Julai 10 ambapo jumla ya wananchama 58 wamejitokeza kuchukua fomu ya ubunge na 61 wamejitokeza kuchukua fomu ya uwakilishi kwa majimbo yote Unguja na Pemba.

 “Kwa unguja pekee majimbo yote ya Uchaguzi ambayo ni 32 wananchama wamejitokeza kuchukua fomu za kuomba ridhaa kuchaguliwa na chama chetu kugombea nafasi ya uwakilishi na ubunge” alisema Said Mzee Said.

 Alisema kwamba muitiko ni mkubwa sana kwa wannchama hao kujitokeza kuchukua hizo fomu ukilinganisha vna miaka iliyopita ambapo wanachama wa chama hicho wamehamasika kujitokeza kuchukua fomu.

 “Kundi kubwa la vijana, wanawake kwa mwaka huu wamehamasika kuchukua fomu za kuomba ridhaa katika chama chetu kuteuliwa kuwa wagombea ambao watatyuakilisha katika uchaguzi Mkuu hapo baadae mwaka huu”alisema Said Mzee said.

 Pia alisema kwamba baada ya kukamika kwa zoezi hilo la uchukuaji fomu vikao mbalimbali vya kamati maalum za chama hicho vitanza kukaliwa kwa siku ya Jumatano Julai 14 kwa lengo la kuwajadili na kuwachuja wagombea hao.

 “Kuanzia kesho siku ya JumaTano Julai 15 kwa wilaya mjini tutaanza kukaa vikao maalum katika Ukumbi wa Ikhilas, na hapa ofisi vikao vitakaa kukaliwa kwa lengo la kuwapitisha hao wagombea na kuanza mchujo”alisema Mwenyekiti Said Mzee Said.

 Hata hivyo alisema kuwa zoezi la uchukuaji wa fomu za udiwani kwa wadi zote unguja na pemba linaendelea ambapo lilianza tangu Julai 11  na linatarajiwa kufika tamati Julai 17 mwaka huu.

 alisema mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo kura za maoni na kamati tendaji kanda kuanzia Julai 20 hadi 23  na Julai 24 kamati tendaji kuteuwa wagombea wa nafasi hiyo.

 Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo alisema kwamba Chama Cha Demokrasia na Maendeleo wamejipanga Katika kuwatumikia Wazanzibar kwa nafasi zote na kwa uwaminifu Mkubwa na Uzalendo wa hali ya juu.

  

“Mwisho nataka niwaambie ndugi zangu Waandishi wa Habari kuwa Chadema tumejipanga kwa asilimia kubwa iwe Jimbo,wadi na hata Taifa tutawatumikia kwa Uzalendo Mkubwa” alisema Said Mzee Said.