Katibu Mkuu CCM: Tusifurahie Benard Membe Kufukuzwa, Milango Iko Wazi Kama Atakiri Makosa na Tutampokea

Katibu
Mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Dkt Bashiru Ally, amemuomba aliyewahi
kuwa Waziri wa Mambo ya Nje Bernard Membe, aache kutapatapa na kwamba
anahitaji kufanyiwa ushauri wa kisaikolojia ili aweze kuwa sawa.


Dr
Bashiru Ameyasema hayo wakati akizungumza  katika mahojiano yake na
Gazeti la Mwananchi leo tarehe 2 Machi 2020 jijini Dar es Salaam

Amesema CCM wamechukua hatua hiyo baada ya hatua za awali kushindwa kufanikiwa….

“Ndugu
Membe alishawahi kupewa adhabu ya onyo kali ikiwa ni hatua ya kujaribu
kumpa nafasi ya kujirekebisha, lakini ilishindikana,  huu ni uamuzi
mgumu tuliochukua, na si kusherehekea na nisingependa WanaCCM kujitokeza
hadharani kufurahia.


Nadhani tumpe muda, ni binadamu ana haki zake,  anahitaji ushauri
nasaha, maana siyo tatizo dogo hili na mimi sitaki kulizungumza kwa
ushabiki hata lingenipata mimi ningehitaji marafiki zangu wa karibu
niwashirikishe” amesema Dkt Bashiru.
 

Dk. Bashiru ameeleza kuwa, milango ya CCM  kupokea wanachama wanaokiri makosa yao na kuomba msamaha iko wazi, hivyo Membe anaweza kukata rufaa juu ya suala hilo.

“Mchakato huu ni kama wa kimahakama kuna rufaa, nikianza mimi kusema wakati mimi ndio nitapokea rufaa kama nipo ni kama naingilia mchakato wa haki. Na matarajio yangu ni kwamba atarudi CCM, nikiwa hai au nimekufa.

“Sababu milango ya kuwapokea wanachama iko wazi na kuondoka iko wazi,
mimi nimesaini barua za misamaha 14 na niko tayari kusaini ya 15 ambayo
ni ya Membe kurudi kama akitaka,” amesema Dk. Bashiru.