UJUMBE WA WABUNGE KUTOKA FINLAND WATUA TANGA KWA ZIARA YA SIKU TATU


Mmoja wa Wabunge wa nchini Finland kushoto akitate jambo na Mkuu wa
Mkoa wa Tanga Martine Shigella leo mara baada ya kumtembelea ofisini
kwake katikati ni Mkuu wa wilaya ya Tanga Thobias Mwilapwa

 Mmoja wa wabunge hao akimuuliza swali mkuu wa mkoa wa Tanga Martine Shigella ambaye hayupo pichani

 Mkuu wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella kushoto akiwa na mmoja wa wabunge kutoka nchini Finland kulia wakiteta jambo

 MKUU wa Mkoa wa Tanga akiwa kwenye picha ya pamoja na ujumbe huo mara baada ya kuzungumza nao

 Sehemu ya ujumbe wa Wabunge kutoka nchini Finland wakiingia kwenye Kituo cha Kulea Watoto wenye ulemavu cha (YDCP) Jijini Tanga wakiongozwa na Mratibu wa Kituo hicho Leopodi Abeid kushoto aliyevaa suti nyeusi

 Mratibu wa Kituo hicho Leopodi Abeid akiwaongoza ujumbe huo kuingia kwenye kituo hicho

Mmoja wa wajumbe hao wakisaini kitabu cha wageni kwenye kituo hicho mara baada ya kukitembelea

 Ujumbe huo wakipata maelezo kutoka kwa mmoja wa wataalamu wa mambo mbalimbali kwenye kituo hicho

UJUMBE
wa Wabunge kutoka nchini Finland wametua nchini kwa ziara yao ya siku
tatu mkoani Tanga na Visiwani Zanzibar ambapo watatembelea miradi
inayofadhiliwa na Serikali ya Finland.
 

Miradi
ambayo watatembelea ni kwenye maendeleo ya Jamii, miradi ya watu wenye
ulemavu  jinsi ya kuwasaidia ili waweze kujiingiza kwenye shughuli za
kimaendeleo na hatimaye kuweza kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza
wakati ujumbe huo ulipokwenda kukutana naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Martine Shigella aliwashukuru kwa kuchagua kutembelea mkoa huo kwa
sababu hapa nchini kuna mikoa mingi.

Mkuu huyo wa mkoa
aliwaambia ujumbe huo kwamba mkoa huo ni miongoni mwa mikoa inayozalisha
kilimo cha Korosho Matunda na Mkonge ambapo kwa asilimia kubwa mkonge
unapatikana mkoani hapa hivyo wanaweza kwenda kuiona ili waweze kuwa
mabalozi wazuri.

Aidha mkuu huyo wa mkoa alisema kwamba mkoa huo
unazalisha matunda kwa wingi na hivi sasa wanatengeneza mazingira
mazuri kwa wawekezaji kuja kuwekeza viwanda vya matunda kwa kufanya
uzalishaji ambao utakuwa na tija kwa wakulima.

“Kwa sasa
wakulima wanazalisha kiasi kikubwa cha matunda lakini tunapata soko dogo
kutokana kutokuwepo kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo kukosekana
kwa viwanda hivyo ninaamini kwamba aina hii ya mahusiano itakuwa na tija
siku za mbeleni”Alisema

“Lakini pia niwaambie kwamba wananchi
wa mkoa wa Tanga ni wakarimu sana hivyo mnaweza kuwashawishi wawekezaji
kwenye maeneo mnayotoka wakaja kuwekeza kwani kuna mazingira rafiki kwa
uwekazaji”Alisema

Hata hivyo Mkuu huyo wa Mkoa alikishukuru
kituo cha Kulea Watoto wenye ulemavu cha (YDCP) kutokana na kuona namna
nzuri ya kuhakikisha watu wenye ulemavu wapata elimu na hivyo kuweza
kujitegemea.

“lakini pia tunawashukuru FIDA kwa msaada wenu kwa
kuwasaidia watoto hao na kuwaonyesha namna mnavyowajali vijana hao kwani
umewasaidia watoto wanatoka kwenye mazingira magumu kuweza kupata elimu
kutokana na ukata unaozikabili familia zao hivyo sisi kama serikali
tunashukuru sana”Alisema RC Shigella.

RC Shigella alisema kwa
sasa serikali inatengeneza mazingira mazuri ya kuwawezesha ofisi zote za
umma zinakuwa mazingira wewezeshi kwa watu wenye ulemavu.

“Mtazamo
wa watu wa Tanga kuhusu watu wenye ulemavu umebadilika hivi sasa
kutokana na kazi kubwa inayofanywa na FIDA,Kanisa na kituo cha YDCP
tunashukuru tutaendelea na ushirikiano huo na utakuwa mzuri na
tunashukuru na kutambua mchango wetu”Alisema

Awali akizungumza
Mratibu wa Kituo cha YDCP Leopodi Abeid leo wamepokea wageni kutoka
Finland ni marafiki wa kanisa la FCT wanaosaidia katika miradi
mbalimbali hapo Tanga wanasaidia kituo cha watoto walemavu kutoka mwaka
2006.

Alisema kwamba serikali ya Finland wamewatuma wabunge hao
kuja kujionea kwa macho shughuli zinafanyika hapa nchini na watazunguka
kwenye miradi yote na watapata taarifa za miradi hiyo ili watakaporudi
waweze kuwasilisha walichokiona.

Mratibu huyo alisema kwamba
katika msafara huo wamekuja wawakikishi wa wabunge wenzao wamekuja wanne
ambao wameambatana na Afisa Mshauri wa miradi ya FIDA kwa ukanda wa
East Afrika anakaa Nairobi.

Hata hivyo alisema pia kwenye
msafara huo wapo pia Afisa kutoka Konga, Mshauri na Meneja wa Mradi
Tanzania ambaye yupo Arusha wameandamana na Afisa miradi FCT makao makuu
Mchungaji Jackson Muna na Afisa wa Mambo ya Afya na hedhi salama
Jackson Senyu kutoa Fida Arusha.

MKUU wa Mkoa wa Tanga Martine Shigella akizungumza na UJUMBE wa Wabunge kutoka nchini Finland wametua nchini
kwa ziara yao ya siku tatu mkoani Tanga na Visiwani Zanzibar ambapo
watatembelea miradi inayofadhiliwa na Serikali ya Finland.