Msumbiji, kenya na tanzania zaanzisha mradi wa kukusanya takwimu za samaki

Miongoni mwa samaki wanapatikana ukanda wa nchi za Kenya, Tanzania na Msumbiji

Nchi tatu za ukanda wa Magharibi wa Bahari ya Hindi Tanzania, Kenya
na Msumbiji zimeanzisha Mradi wa Ukusanyaji Takwimu za Samaki kwa Ukanda
wa Afrika Mashariki (Fidea) ili kuwa na taarifa za pamoja
zitakazosaidia kulinda na kujua hali ya viumbe hao. 

Katika kikao cha pamoja cha kujadili mradi huo, wadau kutoka nchi
wanachama wameshiriki kutoa maoni yao kuhusu mradi huo unaofadhiliwa na
nchi ya Ujerumani. 
Takwimu hizo zitakusanywa kwa njia ya kiteknolojia katika timu ya
wasimamizi wa nchi zote tatu halafu zitachakatwa na kupata habari
zitakazosaidia kufanya uvuvi endelevu. 
Wanachama wameeleza madhara ya kutokuwa na takwimu za samaki ni
kuisha kwa rasilimali hizo huku washiriki wakitolea mfano wa Canada
Mashariki kuwa wamezuia shughuli za uvuvi kwa miaka 30 kwa uvuvi
uliopitiliza bila ya kuwa na kumbukumbu
.