Maadhimisho ya siku ya afya ya mimea duniani yamefanyika jana jijini arusha.

 Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Mimea Duniani yaliyofanyika Jijini Arusha, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu TPHPA Hilda Kinanga_

Egidia Vedasto 

Arusha

Maadhimisho ya siku ya Afya ya  Mimea Duniani imeadhimishwa Kitaifa Jijini Arusha ambapo Mamlaka ya afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania TPHPA kwa kushirikiana na Wadau wa Kilimo wamejipanga kikamilifu kukabiliana na changamoto za  Mabadiliko ya Tabia ya Nchi pamoja na ukuaji wa teknolojia.

Akifunga maadhimisho ya Siku ya Afya ya Mimea  Duniani Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu TPHPA Hilda Kinanga, Kwa Niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Gerald Mweli amesema Wizara hiyo inatambua umuhimu wa Siku ya Afya ya Mimea kwani ndio msingi wa maisha.

Aidha ameongeza kuwa idadi ya watu inazidi kuongezeka duniani, hivyo mabadiliko ya kidijiti katika sekta ya kilimo yanatakiwa kukua kwa kasi kulingana na ukuaji wa idadi ya watu.

“Nawasihi tuwe na ushirikiano katika utendaji kuhakikisha tunailinda afya ya mimea, kupambana na visumbufu lakini pia kuwa makini katika matumizi ya teknolojia mipakani wakati wa kuingiza na kutoa mazao ili kuepuka ongezeko la visumbufu” ameeleza Kinanga.

_Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania TPHPA Profesa Andrew Temu_

Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya  Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania TPHPA Profesa Andrew Temu amesema Mamlaka hiyo inaendelea kuwashawishi vijana ambao ndio kundi kubwa la watu Diniani kwa mujibu wa Sensa kushiriki kilimo kwani kilimo ni biashara.

“Prof Temu amesema TPHPA kwa kushirikiana na wadau wengine wataendeleza ushirikiano   wa kuhakikisha wanainua sekta hiyo na kufafanua kuwa uzalishaji wa mazao umeongezeka kwa asilimia 65 kukidhi matakwa ya malighafi  katika viwanda vyetu” ameeleza  Prof Temu.

Mkurugenzi Mtendaji wa  Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania TPHPA Profesa Joseph Ndunguru wa kwanza (kulia) akiwa na Viongozi wengine katika maadhimisho ya Siku ya Afya ya Mimea Duniani

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Tanzania TPHPA Profesa Joseph Ndunguru ameeleza kuwa maadhimisho hayo yana lengo la kuleta umakini katika ulimwengu kutokomeza maisha duni, kupunguza umaskini na kulinda Bioanuai.

“Sisi kama TPHPA tunaendelea kushughulikia changamoto mbali mbali zinazoikabili afya ya mimea ikiwemo visumbufu kwa maana ya wadudu, kufuatilia usalama wa mipaka na kupambana na Mabadiliko ya Tabia ya Nchi na ninatambua mchango wa Shirika la Chakula na Kilimo Duniani FAO kwa ushirikiano wao mkubwa ambao wamekuwa wakitupatia ikiwemo ushauri katika utendaji kazi wetu” ameeleza Prof Ndunguru.

Sambamba na hayo Mwakilishi wa Shirika la Chakula na Kilimo Umoja wa Mataifa FAO Dk Monday Ahons, katika  hotuba yake ameeleza kwamba afya ya mimea ndio afya ya watu na kuihimiza jamii kutunza mazingira na bioanuai kwa ujumla kwa mustakabali wa uhai wa maisha ya Mwanadamu.

“Nafafanua utambue kuwa mimea ni maisha na furaha pia, kwani mimea hutupa chakula, dawa na pesa, Sisi FAO tutaendelea kushirikiana na TPHPA katika kuhakikisha tunailinda Afya ya Mimea Duniani” amesema Dk Monday Ahons.

Wanafunzi na Wadau wengine wameshiriki katika maadhimisho ya Siku  ya Afya ya Mimea na Viuatilifu Duniani, na kufanyika Kitaifa Jijini Arusha_

Maadhimisho hayo yamefanyika jana katika viwanja vya Makumbusho Jijini Arusha vikishirikisha wadau mbalimbali kama  FAO, WFP, WHO, EPA na wadau wengine yakibeba kaulimbiu “Afya ya Mimea, Biashara Salama na Teknolojia za Kidijitali”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *