Madaktari upasuaji magonjwa ya moyo kutoka israel wavutiwa na bonde la ngorongoro

Baadhi ya madaktari bingwa wa upasuaji magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka Israel wakiangalia utamaduni wa kabila la Wamaasai walipotembelea hivi karibuni Mamlaka ya Hifadhi ya Ngongogoro (NCAA)  

Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk. Fredy Manongi akitoa maelezo ya aina ya vivutio vinavyopatikana Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kwa Madaktari watalii kutoka nchini Israeli walipomtembelea ofisini kwake

Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk. Fredy Manongi (kulia), akijadiliana jambo na baadhi ya madaktari kutoka nchini Israeli waliopata mwaliko wa Rais Dk. John Magufuli kutembelea Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).

Kamishna wa Uhifadhi Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA), Dk. Fredy Manongi akizungumza na wanahabari mara baada ya kufanya mazungumzo na jopo la Madaktari bingwa wa upasuaji magonjwa ya moyo kwa watoto wadogo. 

Baadhi ya wakazi wa boma la Erelai lililomo ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro wakitoa burudani kwa jopo la Madaktari bingwa wa upasuaji magonjwa ya moyo kwa watoto waliotembelea eneo hili kujionea utamaduni wa kabila la Maasai.

Madaktari bingwa wa upasuaji magonjwa ya moyo kwa watoto kutoka nchini Israel wakichukua kumbukumbu ya picha kutoka kwa mkazi wa Boma la Erelai aliyekuwa akiwasha moto kwa njia za asili ndani ya Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro walipofanya ziara yao hivi karibuni.