Na Mapuli Misalaba, Shinyanga
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha
mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko amewaasa viongozi
na wanachama kuendelea kushirikiana katika shughuli mbalimbali za
maendeleo ili kuimarisha jumuiya hiyo.
Ametoa kauli hiyo leo Mei 11,2023 katika ziara yake ya
kamati ya utekelezaji ya umoja wa wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini iliyolenga kutembelea
na kukagua uhai wa chama kwenye kata ya Ibadakuli pamoja na kata ya Kolandolo
ambapo Mwenyekiti huyo amesisitiza umoja ili kuijenga jumuiya na kuleta
maendeleo katika jamii.
Bwana Mrindoko amewaomba viongozi na wanachama
kuanzisha miradi itakayowanufaisha wao na jumuiya kwa ujumla huku akisisitiza
umoja na kuepuka migogoro ili kufikia mipango iliyokusudiwa na jumuiya hiyo.
Amesema ni muhimu viongozi wa jumuiya hiyo kata
kusimama imara katika usimamizi wa ilani ya CCM na kwamba wasikatishwe tamaa na
watu wenye nia mbaya na maendeleo yanayoletwa na viongozi wa serikali kwenye jamii na Taifa kwa ujumla.
“Tusiwe
jumuiya ya kudharaulika tunataka iwe jumuiya ya maendeleo niwaomba wana jumuiya
ya wazazi msikate tamaa kwahiyo tushirikiane katika shughuli hizi za maendeleo
lakini niwaomba tubuni miradi kuanzia kwenye matawi na kata tuwe na miradi ya
kujisimamia sisi wenyewe tusimame imara katika hili”.
“Niwaomba
tupendane, tuwe kitu kimoja, tushikamane tusigombane sisi kwa sisi kama
tukifanya hivo hakuna jambo litafanikiwa tusiupoteze umoja wetu uchaguzi
ulishapita sasa hivi ni wajibu wetu kushikamano, kupendana tukifanya hivo
tutaijenga jumuiya yetu”.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga
mjni Bi. Doris Yotham Kibabi amesisitiza
juu ya uhai wa jumuiya kwenye matawi na kata kwa ujumla kuhakikisha viongozi
wanaongeza au kusajiri wanachama wapya kwa
lengo la kuimarisha ama kudumisha jumuiya hiyo.
Katibu huyo Bi. Doris Kibabi amewakumbusha viongozi na
wanachama wa jumuiya hiyo kuendelea kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita
inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Samia Suluhu
Hassan ambapo amewasisitiza pia kutokuwa kwenye sehemu ya kukwamisha maendeleo
katika miradi inayotekelezwa na viongozi wa kata, wilaya ya Taifa kwa ujumla.
“Kitu
cha kwanza mnatakiwa kwenda kusimamia uhai wa jumuiya kata hii wanachama
waliosajiriwa ni wachache mno, mnatuvunja moyo fanyeni vikao vya ndani ninyi
makatibu wa matawi mtatue hii changamoto lakini niwaombe tuache makundi kwenye
chama chetu tuwe kitu kimoja tushirikiane”.amesema katibu
wazazi Wilaya
“Serikali
inajengwa na wanachama wa chama cha mapinduzi pamoja na wananchi wetu lakini
tujivunie mafanikio ambayo yanaletwa na viongozi wetu wa serikali inayoongozwa
na Mama Samia lakini pia juhudi za Mbunge, juhudu za madiwani kwahiyo pale
ambapo inatakiwa nguvu ya wananchi tushirikiane, tuwe wa kwanza kuhamasisha
maendekleo tusiwe wa kwanza kukwamisha maendeleo tunakosea sisi ndiyo
tunatakiwa tuiunge mkono serikali yetu kufanikisha mambo mbalimbali”.amesema
katibu Bi. Doris
Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya utekelezaji
jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe amewaomba
wazazi na walezi kusimamia maandili kwa watoto kwa kuhakikisha wanatimiza wajibu
wao ili kuwaepusha na wimbi la mmomonyoko wa maadili pamoja na ukatili katika
jamii.
“Wazazi
tunatakiwa tuwe na uchungu ukisikia jambo la ukatili kuna watu wanataka
kulikwamisha lisiende mbele wewe uwe wa kwanza kulipigia kelele kwa ngumu kwa
sababu ndiyo jukumu la mzazi”.
“Tukemee
mapenzi ya jinsia moja kwenye jamii yetu tuwalinde watoto wetu tusiwalaze na
wageni chumbani tuwape elimu watoto na tuwafanye kuwa marafiki ili wakifanyiwa
ukatili hata kule shuleni atakwambia mapema bila uoga tupambane kuupinga ushoga
pamoja na uzagaji tusiruhusu shetani apite kwenye familia yetu”.
Nao baadhi ya viongozi na wanachama wa jumuiya ya
wazazi kata ya Ibadakuli pamoja Kolandoto wameipongeza kamati ya utekelezaji
jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini kwa kufanya ziara hiyo ambapo
wameahidi kuzingatia maelekezo yote yaliyozungumzwa na viongozi hao.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha
mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akizungumza kwenye
ziara hiyo kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.
Viongozi mbalimbali.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga
mjni Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza
na jumuiya ya wazazi kata ya Ibadakuli Manispaa
ya Shinyanga leo Mei 11,2023 wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji Wilaya.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi
Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe akizungumza na jumuiya ya wazazi
kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.

Wilaya ya Shinyanga mjini Daniel Kapaya akizungumza
na jumuiya ya wazazi kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi
Wilaya ya Shinyanga mjini Zulfa Hassan akizungumza
na jumuiya ya wazazi kata ya Ibadakuli Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.
Diwani wa viti maalum kata ya Ibadakuli Mhe. Zuhura
Waziri akizungumza leo kwenye ziara ya kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi
Wilaya ya Shinyanga mjini katika kata hiyo.
Diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Malale akizungumza leo kwenye ziara ya kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi
Wilaya ya Shinyanga mjini katika kata hiyo.
Diwani wa kata ya Ibadakuli Mhe. Msabila Malale, kulia
ni Diwani viti maalum kata ya Ibadakuli Zuhura Waziri.
Mwenyekiti wa CCM kata ya Ibadakuli Bwana Antony
Makwaya akizungumza leo katika ziara hiyo ya kamati ya utekelezaji jumuiya ya
wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha
mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akizungumza kwenye
ziara hiyo kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akisisitiza juu ya usajiri wa wanachama wapya kata ya Kolandato.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi kupitia chama cha mapinduzi CCM, Wilaya ya Shinyanga mjini Bwana Fue Mrindoko akisisitiza juu ya usajiri wa wanachama wapya kata ya Kolandato.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Mhandisi James Jumbe akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjni Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023 wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji Wilaya.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjni Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjni Bi. Doris Yotham Kibabi akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023 wakati wa ziara ya kamati ya utekelezaji Wilaya.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Daniel Kapaya akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.
Mjumbe wa kamati ya utekelezaji jumuiya ya wazazi Wilaya ya Shinyanga mjini Bi. Mary Makamba akizungumza na jumuiya ya wazazi kata ya Kolandoto Manispaa ya Shinyanga leo Mei 11,2023.