Na Seif Mangwangi, Arusha
Kituo Cha uwekezaji Tanzania (TIC), kimeanza kuelimisha wadau wake mabadiliko yaliyomo katika Sheria Mpya ya Uwekezaji Na. 10 ya 2022 ikiwemo kushushwa kwa mtaji wa uwekezaji kutoka Dola100,000 hadi Dola 50,000 kwa mwekezaji wa ndani.
Mkuu wa Kituo cha uwekezaji Kanda ya Kaskazini Daudi Riganda akieleza malengo ya warsha hiyo iliyokutanisha wadau wa Taasisi za Serikali za Jiji la Arusha zinazohusika na uwekezaji |
Akizungumza kwenye warsha ya siku moja iliyoandaliwa na kituo hicho Kanda ya Kaskazini, Mkuu wa Kituo hicho Daudi Riganda amesema kituo kimeamua kualika taasisi zote zinazowezesha uwekezaji mkoani Arusha ili kujua sheria hiyo na kuweka mikakati ya kuhudumia wawekezaji kwa ufanisi na kwa wakati.
Amesema uendeshaji wa Warsha hiyo ni utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Kituo Cha uwekezaji sambamba na utekelezaji wa Sheria ya Uwekezaji inayokitaka Kituo kushirikiana na taasisi za Serikali ambazo ni Wizara, Idara na Wakala.
” Warsha hii ilikusudia kujifunza namna taasisi zinazohudumia uwekezaji zinavyohudumia wawekezaji katika maeneo yao, kujadiliana kuhusu changamoto mbalimbali zinazokabili utoaji huduma kwa wawekezaji na kupendekeza namna ya utatuzi wa changamoto hizo,” amesema.
Amezitaja Taasisi zilizoshiriki Warsha hiyo ni pamoja na Tanzania Plant Health and Pesticides Authority (TPHPA), NEMC, TMDA, TBS, Government Chemist Laboratory Authority (GCLA), Tanzania Atomic Energy Commission (TAEC), Uhamiaji na ofisi ya Afsa Kazi.
Taasisi zngine ni TRA, NIDA, OSHA, WMA, Arusha Urban Water Supply and Sanitation Authority (AUWSA), TANESCO, Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Mkoa, Ofisi ya Msajili wa Hati Mkoa, Hamalshauri ya Wilaya ya Arusha, Benki Kuu ya Tanzania, Bonde la Maji Pangani, na TARURA pamoja na wawakilishi kutoka sekta binafsi za TAHA na TATO.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa Warsha hiyo Mkuu wa Wilaya ya Arusha Felician Mtahengerwa amezitaka taasisi hizo kusaidia wawekezaji badala ya kuwa wakwamishaji, na kwamba endapo mwekezaji
Mkuu wa Wilaya ya Arusha akifungua warsha ya sikuoja ya wadau wa uwekezaji taasisi za Serikali Mkoa wa Arusha |
atashindwa kuridhika na huduma zinazotolewa au kukwamishwa anaweza kuhama mkoa au hata nchi ili kwenda kule ambapo atahudumiwa kwa haraka na kwa ubora unaotakiwa.
Aidha, amezitaka taasisi hizo kutojifungia kwa kigezo cha sheria zao, bali wasomame na kushirikiana kwa vile taasisi zote hizo zinafanya kazi Moja.