Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu akimuaga mgeni rasmi mhifadhi wa hifadhi ya Taifa ya Manyara, Neema Mollel mara baada ya kufungua mkutano maalum wa APC |
Wa kwanza kulia ni Mhifadhi Mkuu wa hifadhi ya Taifa ya ziwa Manyara Neema Mollel wakifanya mazungumzo na Mwenyekiti wa APC Claud Gwandu pamoja na wanachama wengine |
Na Seif Mangwangi, Arusha
Watanzania wametakiwa kutumia likizo ya siku kuu ya christmass na mwaka mpya kutembelea hifadhi za Taifa na kujionea wenyewe maajabu na vivutio vilivyopo katika hifadhi hizo.
Wito huo umetolewa jana Disemba23, 2022 na mhifadhi Mkuu katika hifadhi ya Taifa ya Ziwa Manyara Neema Mollel alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu Maalum wa waandishi wa habari wanachama wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha (APC).
Neema amesema maeneo ya hifadhi ni urithi ambao watanzania wamepewa bure na Mungu hivyo ni wakati muafaka kwa watanzania kutumia likizo ya mwaka kutembelea hifadhi hizo na kupata mapumziko sahihi.
Wanachama wa APC wakifuatilia mjadala wa mabadiliko ya katiba |
Amesema hifadhi ya ziwa Manyara ni miongoni mwa hifadhi zenye vivutio vingi ambavyo watanzania wanapaswa kuviona badala ya kuachia wageni pekee waweze kutembelea hifadhi hizo.
” Hifadhi ya Manyara ni moja ya hifadhi rahisi sana kufikika, ukiwa Arusha mjini ni kilometa chache sana unaweza kutumia hadi kufika katika hifadhi yetu na gharama zetu ni ndogo sana,”amesema
Mratibu wa APC, Seif Mangwangi akiwasilisha maeneo ya katiba ambayo yanapendekezwa kufanyiwa mabadiliko katika mkutano Mkuu Maalum wa APC, uliofanyika katika hifadhi ya Manyara |
Awali akimkaribisha mhifadhi wa Manyara, Mwenyekiti wa APC, Claud Gwandu amesema waandishi wa habari ni miongoni mwa wadau wakubwa wanaopaswa kutembelea hifadhi za Taifa na kuzitangaza.
Amesema Waandishi wa habari ni miongoni mwa waandishi ambao wamekuwa wakitoa kipaumbele kutangaza hifadhi za Taifa na kwamba mbali ya kufanyika kwa mkutano huo pia wamepata fursa ya kutembelea hifadhi ya ziwa manyara na lengo ni kutangaza vivutio vilivyopo.
Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Arusha Claud Gwandu akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa mkutano Mkuu Maalum wa mabadiliko ya Katiba |
” Mhifadhi napenda kukuhakikishia kuwa mara baada ya mkutano huu tumejipanga kutangaza hifadhi ya Manyara kupitia vyombo mbalimbali vya habari, hapa tuko waandishi zaidi ya 40 kwa hiyo tegemea kuona habari nyingi katika vyombo nyetu vya habari,”amesema.