Benki ya cba yaanza kutoa mikopo ya ujenzi

Na Vero Ignatus,Arusha
Benki
ya Biashara Afrika (CBA ) imeanza  kutoa mikopo ya ujenzi kwa ajili
ya  kuwawezesha wateja wake kuweza kujenga na kumiliki nyumba kwa kupata
mkopo rafiki ambao utawawezesha kujenga na kulipa kwa urahisi.

Akizungumza katika siku maalumu ya Wateja wa benki hiyo (customers day)  Mkurugenzi
wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko amesema kuwa wanatoa mikopo ya
ujenzi  kulingana na uwezo wa mteja kulipa mkopo ,pia kulingana na faida
anazozipata mteja katika biashara yake ,mkopo huo  umeangalia mahitaji
ya wateja wao ya  kumiliki nyumba za ndoto zao.

Kwa
sasa pia tuna mikopo maalumu kwa Wafanyakazi walioko serikalini ili
waweze kunufaika na fursa za mikopo iliyoko katika benki zetu” Anaeleza
Mkurugenzi huyo
Anasema
kuwa wameanzisha huduma maalumu kwa ajili ya watalii kupata huduma za
kifedha kubadilisha fedha za kigeni pamoja na huduma nyingine za
kifedha.
Mkuu
wa Idara ya wateja binafsi ,Julius Konyani anaeleza juu ya  siku ya leo
ambayo wanakutana na wateja wetu tunawashukuru kwa biashara
wanayotupatia na kupata mrejesho juu yale ambayo benki yao inafanya.
Julius
alisema kuwa Wateja wao wanahitaji makazi ya kudumu walihitaji kuwa na
viwanja na kuanza ujenzi ,tunawakopesha mkopo wa kununua viwanja na
kujenga wanaulipa kwa miaka 20.

 Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko akizungumza na wateja waliohudhuria katika siku hiyo maalum 
 Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko akifafanua jambo kwa wateja waliohudhuria kwa siku maalumu ya mteja  Benk hiyo.
 Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko na wafanyakazi wa Bank hiyo.
 Picha ya pamoja ya wafanyakazi wa Benki ya CBA .
 Mkutano unaendelea .
 Wafanyakazi na wayeja wakifiatilia kwa makini kile kinachoendelea katika mkutabo huo.
Wateja wa CBA Bank wakifuatilia mkutano kwa makini.
Mkurugenzi wa Benki ya CBA ,Dr.Gift Shoko akimkabidhi zawadi ya Tv mmoja wa wateja wa wateja wa Bank hiyo.