Afisa Masoko na Mahusiano wa shirika la TEMDO, Dkt.Sixty Mmasi akizungumza na wageni waliotembelea banda lao katika maonyesho ya Sido yanayoendelea Jiji la Arusha |
Na Queen Lema Arusha
Taasisi ya uhandisi na usanifu wa mitambo(Temdo) imefanikiwa kubuni teknolojia mbadala ya kukausha zao la mihogo kwa muda mfupi huku mihogo hiyo ikifanikiwa kubaki na virutubisho ambavyo vinatakiwa
Kwa Sasa wakulima wa zao la miogo mara nyingi wanajikuta wakipata hasara kubwa kutokana na zao hilo kuharibika hasa kwenye mchakato wa ukaushaji
Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana kwenye maonesho ya SIDO yanayoendelea jijini Arusha Afisa mausiano na masoko wa TEMDO Dkt Sixbert Mmasi alisema kuwa teknolojia hiyo ni zao jipya la uvumbuzi ambao kila mwaka taasisi hiyo inabuni
Akiongelea teknolojia hiyo alisema kuwa hapo awali wakulima wa zao la miogo walikuwa wanalazamika kutumia siku nyingi katika kukausha mihogo hali ambayo wakati mwingine inaharibika
Dkt Mmasi alisema kuwa uwepo wa teknolojia utaweza kuwaraisishia kazi wakulima wakati wa usindikaji kwani watalazimika kutumia siku moja pekee tofauti na hapo awalia ambapo walikuwa wanatumia siku zaidi ya 10 Huku wakitumia nishati kama jua kama chanzo Cha ukaushaji
“Kwa kutumia teknolojia hii mkulima ataweza kuvuna mhogo wake na akaukausha siku hiyo hiyo na akaweza kufungasja unga katika vifungashio tayari kwa matumizi ya nyumbani Mimi nadhani kuwa huyu ni mkombozi mkubwa sana na Sasa tutaweza kutoa thamani halisi ya zao Hilo la mhogo”alisema
Katika hatua nyingine aliwataka wajasirimali ambao ni wamiliki wa viwanda kuhakikisha kuwa wanatumia uwepo wa taasisi hiyo hasa katika uvumbuzi wa mashine na teknolojia mpya ambazo zote zinalenga kuinua uchumi wa taifa
Alisema kuwa huwa wanawawezesha wadau wa viwanda kwa kuwapa elimu na namna sahihi ya kutumia mashine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ndani ya viwanda.
“Lengo letu ni kuona kuwa sekta hasa ya viwanda inakuwa na mapinduzi makubwa kwa kuwa tuna uwezo mkubwa sana wa kutengeneza vitu ambavyo hapo awali vilikuwa vinazalishwa nje ya nchi Sasa tunazalisha na kubuni kwa umairi mkubwa,niwatake watanzania na wamiliki wa viwanda Sasa kutumia taasisi hii ili tubuni wote kwa pamoja.