Temdo yabuni teknolojia mbadala ya kukausha zao la mihogo

Afisa Masoko na  Mahusiano wa shirika la TEMDO, Dkt.Sixty Mmasi akizungumza na wageni waliotembelea banda lao katika maonyesho ya Sido yanayoendelea Jiji la Arusha

 Na Queen Lema Arusha

Taasisi  ya uhandisi na usanifu wa mitambo(Temdo) imefanikiwa kubuni teknolojia mbadala ya kukausha zao  la mihogo kwa muda mfupi huku mihogo hiyo ikifanikiwa kubaki na virutubisho ambavyo vinatakiwa 

Kwa Sasa wakulima wa zao la miogo mara nyingi wanajikuta wakipata hasara kubwa kutokana na zao hilo kuharibika hasa kwenye mchakato wa ukaushaji 

Akizungumza na waandishi wa habari mapema jana  kwenye maonesho ya SIDO yanayoendelea jijini Arusha Afisa mausiano na masoko  wa TEMDO Dkt Sixbert Mmasi alisema kuwa teknolojia hiyo ni zao jipya la uvumbuzi ambao kila mwaka taasisi hiyo inabuni 

Akiongelea teknolojia hiyo alisema kuwa hapo awali wakulima wa zao la miogo walikuwa wanalazamika kutumia siku nyingi katika kukausha mihogo hali ambayo wakati mwingine inaharibika 

Dkt Mmasi alisema kuwa uwepo wa teknolojia utaweza kuwaraisishia kazi wakulima wakati wa usindikaji kwani watalazimika kutumia siku moja pekee tofauti na hapo awalia ambapo walikuwa wanatumia siku zaidi ya 10 Huku wakitumia nishati kama jua kama chanzo Cha ukaushaji

“Kwa kutumia teknolojia hii mkulima ataweza kuvuna mhogo wake na akaukausha siku hiyo hiyo na akaweza kufungasja unga katika vifungashio tayari kwa matumizi ya nyumbani  Mimi nadhani kuwa huyu ni mkombozi mkubwa sana na Sasa tutaweza kutoa thamani halisi ya zao Hilo la mhogo”alisema 

Katika hatua nyingine aliwataka wajasirimali ambao ni wamiliki wa viwanda kuhakikisha kuwa wanatumia uwepo wa taasisi hiyo hasa katika uvumbuzi wa mashine na teknolojia mpya ambazo zote zinalenga kuinua uchumi wa taifa 

Alisema kuwa huwa wanawawezesha wadau wa viwanda kwa kuwapa elimu na namna sahihi ya kutumia mashine kwa ajili ya matumizi mbalimbali ndani ya viwanda.

“Lengo letu ni kuona kuwa sekta hasa ya viwanda inakuwa na mapinduzi makubwa kwa kuwa tuna uwezo mkubwa sana wa kutengeneza vitu ambavyo hapo awali vilikuwa vinazalishwa nje ya nchi Sasa tunazalisha na kubuni kwa umairi mkubwa,niwatake watanzania na wamiliki wa viwanda Sasa kutumia taasisi hii ili tubuni wote kwa pamoja.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *