Na Doreen Aloyce , Zanzibar
Waziri wa Maji,Nishati na Madini Shahibu Hassan Kaduara wa Visiwani Zanzibar amewataka watumishi wa Wizara hiyo kufanya kazi kwa ushirikiano na juhudi kubwa pamoja na kusimamia nidhamu za watendaji wenzao jambo ambalo litasaidia kupiga hatua zaidi.
Kauli hiyo aliitoa Visiwani hapa wakati alipokuwa kwenye tukio la makabidhiano ya Ofisi baina yake na Waziri aliyekuwepo kwenye Wizara hiyo baada ya kupangiwa Wizara ya uchumi wa Blue na uvuvi na Raisi wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Mwinyi.
Aidha Waziri Kaduara amesema kuwa hakuna jambo jema kama mashirikiano na kama watazungumza lugha moja,Nia moja kazi itakuwa rahisi na badala ya kutawanyikana lengo la Serikali halitafikia.
“Leo nimekabidhiwa Ofsi mpya ninacho waahidi ni ushirikiano uliotukuka kikubwa tuendeleze pale tulipoachiwa na Waziri ambaye amemaliza muda wake na amefanya kazi nzuri ili wananchi wetu waone faida “
“Pia niwaombe mkasimamie nidhamu ya Wataalamu wenzetu tusiende kufukuza mtu,Wala hakuna atakayefukuzwa na hakuna tutakayemuacha Bali turekebishe Tabia zetu ili kujenga ufanisi uliotukuka tukifanya hivyo Tutakuwa wamoja na kufurahia keki hii ambayo tumepewa” amesema Kaduara.
Nae Waziri aliyekuwepo awali Ambaye amehamishiwa Wizara ya Uchumi wa Blue na uvuvi Suleiman Masoud Makame amewaomba watumishi kufanya kazi kwa Umoja na kwamba uko tayari Kutoa ushirikiano,ushauri na maoni pale atakapotakiwa.
“Mimi Niko tayari kufanya kazi nae lile nililoanza nalo na nilipofikia ili tuweze kufikia Adhma ya Serikali , na nimemkabidhi mambo mbalimbali Wizara na mashirika yake ikiwemo miradi inayoendelea mikubwa ukiwemo Mradi mmoja wa Dola 192 na ujenzi wa matanki ambapo “amesema Waziri Suleiman Masoud Makame .
Naibu waziri wa Wizara hiyo Shabani Ally Othuman amesema kuwa Yale yote yaliyotolewa na Waziri yatatekelezwa kiufanisi ili kazi iweze kusonga mbele.