Burian robert mugabe, rais jpm amlilia

Rais 
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Dkt. John Pombe Magufuli
ameeleza kusikitishwa kwake na kifo cha Rais Mstaafu wa Zimbabwe, Robert
Mugabe ambaye ameaga dunia nchini Singapore alikokuwa akipatiwa
matibabu.


Magufuli
kupitia akaunti yake ya Twitter amemwelezea Mugabe kuwa alikuwa
kiongozi shupavu, jasiri ambaye aliupinga na kuukataa ukoloni kwa
vitendo.

“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Rais Mstaafu na Baba wa Taifa la Zimbabwe Mzee Robert Mugabe. 

“Afrika
imepoteza mmoja wa viongozi Jasiri, Shupavu, Mwanamajumui wa  Afrika na
aliyekataa ukoloni kwa vitendo. Mungu aiweke roho yake mahali pema
peponi, Amina.”