Dkt mpango awataka wanahabari kutumia lugha fasaha

 Na Seif Mangwangi, Arusha

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Phillip Mpango amewataka wanahabari kuepuka kutumia lugha isiyo rasmi, na badala yake watumie lugha sanifu na fasaha ili kuwezesha taaluma hiyo kukua.

Akifungua kongamano la siku tano lililoshirikisha watayarishaji wa vipindi,waandishi wa habari na wadau mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi, Makamu wa Rais Dkt Mpango amesema Serikali itaendelea kukuza na kutangaza lugha ya Kiswahili kikanda , Kitaifa na Kimataifa katika kuleta tija kwenye matumizi sahihi ya lugha hiyo kwa vyombo vya habari na radio.

Alisema si jambo jema kuendelea kuandika mipango,sera na mienendo ya hukumu kwa lugha za kingereza bali ziandikwe kwa lugha ya Kiswahili ikiwemo kuongeza vitabu vya kufundishia na kamusi.

Alisema lugha hiyo ni miongoni mwa lugha saba inayotambuliwa na Umoja wa Afrika na inahadhi kutokana na kutambuliwa Kitaifa na Kimataifa

Alisema kongamano hilo la pili linafaida nyingi ikiwemo kuboresha mahusiano mbalimbali na kumpongeza Balozi Shio kwa kukuza lugha ya Kiswahili na alimpongeza Noel Karekezi kwa kazi nzuri aliyofanya kwa kuhakikisha lugha hiyo inatumika akiwemo Balozi Salma Kikwete

Aliwaomba wabunge mapema kabisa kuacha kutumia Kiswanglishi ya Bungeni na alipongeza wanahabari kwa kutumia kongamano hilo kwaajili ya kujadiliana changamoto za kukuza kiswahili ikiwemo kuwezesha idhaa za kiswahili kuwa bidhaa adimu

Alionya ongezeko la upotoshaji wa lugha ya kiswahili hivyo alitoa rai kwa vijana kuandika vitabu vya kiswahili kuwa ufasaha ili kuhakikisha lugha ya kiswahili inakua

Alisisitiza kuwa serikali ipo tayari kupokea na kufanyia kazi maoni na mapendekezo yatakayotolewa katika mkutano huo na kuwa walimu wazuri wa lugha ya kiswahili na kumwagiza Waziri Mchengerwa kushughulikia ombi la kutangaza hatimiliki ya kutangaza vitabu vya kiswahili nchini Tanzania huko Nairobi nchini

Kenya

Alisema uelewa wa Teknolojia ni muhimu katika matumizi ya Tehama na kusisitiza kubadilishana uzoefu na kubadilishana maarifa ili kupata utaalam zaidi katika kutangaza lugha ya kiswahili kuwa ufasaha zaidi

Alipokea tuzo ya heshima ya nishani ya heshima kwa  Rais Samia Hassan Suluhu pamoja na yeye mwenyewe ,alizindua kitabu cha Kiswahili na Maendeleo ya Teknolojia kilichotungwa na Mwandishi Victor Elliah,Kamusi kuu ya Kiswahili.

Waziri wa Utamaduni,Sanaa na Michezo,Mohamed Mchengerwa alisema lugha ya kiswahili kuwa sasa inaenea na kuenezwa kwa kasi kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia

Alisema lugha hiyo imekubalika na kuenea kwasababu ya ubantu wa lugha hiyo sanjari na mchango mkubwa kutoka kwa waasisi wa Taifa hili chini ya Uongozi wa Hayati Mwalimu Julius Nyerere aliyekuwa Rais wa Tanzania kwa kusisitiza kiswahili lazima kitumike katika shughuli zote za kutoa huduma

Alisema fikra za Baba wa Taifa,Mwalimu Nyerere ziliwekwa kwaajili ya kuendeleza kiswahili na Baraza la Kiswahili la Taifa (Bakita)lilifanya kongamano la kwanza Jijini Dar es Salaam na leo hii ni mara ya pili kufanyika

Alisema kongamano hilo ni jambo jema la kupata elimu juu ya matumizi sahihi ya lugha kwani kila kukicha vyombo vya habari vinakuwa kwani kwa sasa kiswahili ni bidhaa hivyo alitoa rai kwa wadau wa kiswahili kuchangamkia fursa za ukalimani, na hivi sasa wizara hiyo ipi mbioni kuandaa kanzi data ya watoa lugha ya kiswahili ili kuwatambua katika kukamata fursa zinazojitokeza nchi mbalimbali

Alisema kila jambo linawezekana iwapo akijipanga hivyo katika kipindi cha uongozi wake matokeo chanya yatafanyika ili kukuza lugha ya kiswahili nje ya mipaka ya Tanzania na kusisitiza wanaipongeza serikali ya awamu ya sita kwa jitihada za kukuza kiswahili ndani na nchi za nje

Alisisitiza kuwa kiswahili kimetangazwa kuwa lugha ya kazi kwa Umoja wa Afrika hivyo wanashukuru kwa hatua hiyo na wanaamini maamuzi hayo yanatoa fursa mbalimbali za kuitangaza lugha hiyo adhimu na kwakutumia Baraza la Kiswahili ( Bakita) na Baraza la Kiswahili Zanzibar (Bakiza) .

Kongamano  la pili la la siku tano la  Idhaa za Kiswahili Duniani liilofanyika Jijini Arusha na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali yenye kauli mbiu isemayo”Tasnia ya Habari kwa Maendeleo ya Kiswahili Duniani”

Naye Balozi wa Tanzania nchini Ethiopia, Innocent Shio na Mwakilishi wa Umoja wa Kudumu wa Afrika , alisema kiswahili kianze kutumika kama lugha ya kazi katika Umoja wa Afrika na kusisitiza kuwa changamoto ya kibajeti kwa umoja huo ambayo ni zaidi ya dola milioni 10 za kimarekani 

Alisema katika kukabiliana na changamoto hiyo Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeamua kuchukua hatua mbalimbali ikiwemo suala la nafasi ya lugha katika utengamano wa bara la Afrika ikiwemo kufanya uzengezi wa kushawishi nchi za Afrika kuunga mkono kiswahili kitumike katika mikutano yote ya kazi

Alisema ushawishi huo katika Umoja wa Afrika umewezesha nchi wanachama kutambua kiswahili kuwa lugha muhimu katika nchi wanachama wa umoja wa Afrika ikiwemo kusisitiza kiswahili kuwa ni lugha ya mawasiliano katika umoja huo

Alisema Rais Samia Suluhu alisisitiza ni muda muafaka kwa nchi ya Tanzania kutumia kiswahili zaidi kama lugha ya kazi ili kuleta uzito na umuhimu wa mtangamano wa kijamii na kiuchumi ili kuleta mafanikio makubwa ya lugha hiyo adhimu

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inachangia dola za kimarekani 250,000 katika kukuza lugha ya kiswahili

Naye Balozi wa Kiswahili nchini Tanzania,Salma Kikwete kongamano hilo ni jitihada za kukuza Kiswahili na kusisitiza lugha zingine zilikuja sababu ya kutugawa kiutawala lakini lugha ya Kiswahili ni lugha yenye misamiati mingi

Alihoji kwanini watanzania wajinyanyapae kuhusu Kiswahili hivyo lazima watanzania watoke huko na kutambua kuwa Kiswahili ni lugha yetu sisi waafrika hivyo ni lazima kujivunia na kuitangaza katika dunia yote

“Lugha ya Kiswahili ni lugha yenye sauti nasibu zinazotumika na watu katika kuwasiliana na kusisitiza kiswahili kinamisimiati mingi lazima tukipe kipaumbele na wanahabari tumieni lugha hii kuitangaza zaidi”

Alisema Kiswahili ni bidhaa hivyo isipotumiwa vizuri wengine wataitumia kwani zile lugha nyingine zimekuja kitutawala na kutupambanua katika utawala lakini lazima tusome lugha hii ya Kiswahili

Naye Mkurugenzi wa Kituo cha Radio ya Sauti ya Injili ya Nchini Kongo,Noel, James alisema kongo wanatumia vipindi vingi vya Kiswahili kutoka nchini Tanzania na aliipongeza nchini ya Tanzania kwa kutumia lugha ya kiswahili ambayo hutumiwa nchini Kongo kama lugha ya nne kati ya lugha 154 zinazotumika nchini mwao