Watakao vujisha mitihani darasa la saba kushtakiwa

Dafroza Ndalichako, Afsa Elimu Mkoa wa Shinyanga

 Na  Mapuli  Misalaba,  Shinyanga

Kamati ya uendeshaji wa mitihani ngazi ya Mkoa katika Mkoa wa Shinyanga imewatahadharisha wasimamizi wa mitihani ya darasa la saba itakayofanyika kesho septemba 8 hadi septemba 9 kutojihusisha na udanganyifu wa aina yoyote na kwamba pale itakapobainika kufanyika hivyo wahusika watachukuliwa hatua kali za kisheria.

Hayo yameelezwa na Afisa elimu Mkoa wa Shinyanga Mwalimu DAFROZA  NDALICHAKO ambapo amesisitiza zaidi kwa wasimamizi na walimu kuepuka kutumia mbinu zozote za udanganyifu kwa lengo la kuwasaidia watahiniwa hao kwa kuwa maandalizi ya miaka saba yatawawezesha kufanya mitihani hiyo kwa kujiamini

“sisi kama kamati ya uendeshaji mitihani ngazi ya  Mkoa  kwa kushirikiana na mwenyekiti wetu ambaye ni katibu tawala Mkoa tumepita katika Halmashauri zote kutoa semina katika suala ya usimamizi na uendeshaji wa mitihani asijitokeze mtu afanye udanganyifu”

“ kunamadhara makubwa kwa mtahiniwa mwenyewe endapo akibainika anafutiwa matokeo lakini kwa mwalimu akipainika amefanya udanganyifu hatua kali za kisheria zitachukuliwa” 

Ndalichako amesema jumla ya wanafunzi 38,695 wa Darasa la Saba katika shule mbalimbali za Msingi Mkoani Shinyanga, kati yao wavulana ni 18,134 na wasichana 20,561  kesho wataanza kufanya mtihani wa kuhitimu elimu ya Msingi 

Afisa elimu huyo amesema kuwa idadi hiyo inajumuisha wanafunzi 36,976 wanaosoma katika   shule zinazotumia mfumo wa kiswahili wakati wanafunzi 1686   wanasoma shule za mfumo wa kiingereza 

“wanafunzi hao wapo katika makundi mbalimbali wapo wale wa mfumo wa kiswahili ambapo idadi yao ni 36976 lakini wapo wa mfumo wa kiingereza ambao ni 1686 lakini tunawatahiniwa wenye uono hafifu wako 29 na mtahiniwa mmoja asiyeona”

Ametoa wito kwa wazazi kutambua  umuhimu wa elimu ya watoto ambapo amesema elimu ni ufunguo wa maisha, elimu ni mali na ni haki ya mtoto “wazazi watambue elimu ya watoto wasiwazuie kufaulu, waziwazuie kufanya mitihani wala kuwapa kazi nyingi za nyumbani siku hizi za mitihani kwani endapo wakimalamesema Ndalichako

Mtihani wa Darasa la Saba utafanyika kwa siku mbili ambapo utaanza kesho Septemba 08 Nchini kote na kumalizika Septemba 09.