Ziara yamhe. mary masanja uwt kwimba

NA MWANDISHI WETU
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mwanza, Mhe. Mary Masanja amefanya ziara katika Jumuiya wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kwimba na kuwataka wanajumuiya hao kushirikiana kuhakikisha umoja huo unakua.
“Ili Jumuiya hii isonge mbele tuwasaidie hawa viongozi waweze kutekeleza majukumu yao” amesema Mhe. Masanja.
Aidha, amewashukuru viongozi wa Wilaya ya Kwimba kwa kuhamasisha mpaka kumuwezesha kufanikiwa kuchaguliwa kuwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mwanza.
Pamoja na shukrani hizo, Mhe. Mary Masanja amekabidhi majiko ya gesi, mtaji wa laki moja kwa kila mwanajumuiya ili kujikwambua kiuchumi ,pikipiki kwa ajili ya biashara ya bodaboda itakayoongeza mapato ya jumuiya na kompyuta itakayosaidia katika utendaji wa shughuli za ofisi.
Mhe. Mary Masanja amehitimisha ziara yake mkoani Mwanza.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mwanza, Mhe. Mary Masanja akikabidhi pikipiki na majiko ya gesi kwa Jumuiya wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kwimba alipofanya ziara katika jumuiya hiyo leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mwanza, Mhe. Mary Masanja akifurahia pamoja na wanajumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kwimba baada ya kuwakabidhi pikipiki, majiko a gesi na kompyuta alipofanya ziara katika jumuiya hiyo leo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mwanza, Mhe. Mary Masanja akizungumza na wanajumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kwimba(hawapo pichani) alipofanya ziara katika jumuiya hiyo leo.
Katibu wa CCM Wilaya ya Kwimba Latifa Malimi akitoa neno la shukrani kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mwanza, Mhe. Mary Masanja (katikati) kwa niaba ya wanajumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kwimba(hawapo pichani) baada ya kukabidhiwa pikipiki, majiko ya gesi, kompyuta na fedha za kuanzisha miradi midogomidogo katika kikao kilichofanyika leo.
Baadhi ya wanajumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Wilaya ya Kwimba wakimsikiliza Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii na Mbunge wa Viti Maalum Mwanza, Mhe. Mary Masanja (hayupo pichani) alipokuwa akizungumza wakati wa ziara yake iliyofanyika leo katika ukumbi wa CCM Wilaya ya Kwimba.