Crdb benki yatoa mikopo ya kilimo ya bilioni 735 nchini

 

Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa
Benki ya CRDB Boma Rabala kushoto akisaini mkataba wa makubaliano 
kati
yao na Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa
Bima ya Afya (NHIF) Makao Makuu Hipoliti Lello kwa ajili ya  Bima ya
Afya kwa wakulima baina ya Benki ya CRDB, NHIF na Vyama vya Wakulima
wa Mkonge (AMCOS)
Halfa ilifanyika wilayani Korogwe

Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa
Benki ya CRDB Boma Rabala kushoto akibalishana mkataba huo

Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) Makao Makuu Hipoliti Lello mara baada ya kutiliana saini

Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa
Benki ya CRDB Boma Rabala kushoto akibadilishana mkataba huo na

Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) Makao Makuu Hipoliti Lello mara baada ya kutiliana saini

MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa
Benki ya CRDB Boma Rabala kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi
Mkurugenzi wa wateja
wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Boma Rabala akizungumza wakati wa halfa hiyo
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akisisitiza jambo wakati wa halfa hiyo kushoto ni Mkurugenzi wa wateja
wadogo na wakati wa Benki ya CRDB Boma Rabala  na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Korogwe Basila Mwanukuzi

Kaimu
Mkurugenzi wa Huduma za Uanachama wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya
(NHIF) Makao Makuu Hipoliti Lello akzungumza wakati wa halfa hiyo

BENKI ya CRDB imetoa mikopo ya Kilimo yenye thamani ya
Bilioni 735 katika mwaka wa fedha 2020/2021 ili kuongeza tija kwenye
uzalishaji  ambayo ni sawa na asilimia 43
ya mikopo ya Kilimo inayotolewa nchini.

Hayo yalisemwa na Mkurugenzi wa wateja wadogo na wakati wa
Benki ya CRDB Boma Rabala wakati wa halfa ya utiliaji wa sahihi wa makubaliano
ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya Benki ya CRDB, NHIF na Vyama vya Wakulima
wa Mkonge (AMCOS)

Halfa ilifanyika katika Ukumbi wa Korogwe Executive na
kuhudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga wa Tanga Adam Malima wakiwemo viongozi
mbalimbali.

Rabala ambaye pia ni Mkurugenzi mwenye dhamana ya uendeshaji
na usimamizi wa Matawi ya Benki hiyo ambaye katika halfa hiyo alimwakilisha Afisa
 Mkuu wa Biashara wa benki ya CRDB kwenye
suala hilo.

Alisema kati ya mikopo hiyo Bilioni 494 imelekezwa kwenye
mazao makuu ya kimkakati hivyo kusaidia zaidi ya Amcos zaidi 472 kupata
mikopo  kwa ajili ya kuongeza tija kwenye
uzalishaji wa kilimo ambapo ni maeneo ya mikopo ya pembejeo ,maghala.

Aliyataja maeneo mengine iliyotolewa mikopo hiyo ni ujenzi wa
viwanda vya kuchakata mazao,mikopo kwa ajili ya miradi ya ufuigaji,uwekezaji
kwenye misitu na mazao yake hasa kwenye maeneo ya uvuvi.

Mkurugenzi huyo wa wateja wa kati na wadogo alisema katika
mikopo hiyo kwa Tanga wamewekeza kwenye zao la Mkonge na wametoa mikopo yenye
thamani ya Bilioni 7.6.

Alisema fedha hizo zilitolewa kwa wakulima wadogo kupitia
kwenye vyama vya ushirika wanaounganishwa kwenye mifumo madhubuti ya kifedha
kupitia mtandao imara wa benki yao na mawakala 
na huduma zao za Simbanking.

Aidha alisema kwamba benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kufufua
ushirika kwa kuongeza mitaji na ili kuhuisha na kujenga ushirika imara na wameweza
kutoa mtaji wa bilioni 3.2 kwa benki ya Kakoba na hivi karibuni walitoa mtaji
wa Bilioni 7 kwa ajili ya Benki ya KCBL hiyo inawezsha kwa benki hizo za ushirika
kuweza kupata mitaji inayofikia bilioni 10.2.

Hata hivyo alisema hayo ni makubaliano kubwa sambamba kwenye
suala la ushirika kuhaikisha mambo yanasonga mbele huku akitoa wito kwa
kuvikaribsha vyama vya ushirika kujiunga na benki ya CRBD kuweza kupata mazingira
wezeshi .

Naye kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ameshuhudia
utiliaji wa sahihi wa makubaliano ya Bima ya Afya kwa wakulima baina ya Benki
ya CRDB, NHIF na Vyama vya Wakulima wa Mkonge (AMCOS) alisema mpango huo ni kwa
sababu unakwenda kuhakikishia uhakika wa matibabu wakulima.

Alisema mkulima mwenye uhakika wa afya yake ni jambo zuri kwa
sababu kupitia mpango wa bima litawawezesha kunufaika na huduma za matibabu
wakati wanapokuwa wakugua.

”Jambo hili ni nzuri kwa sababu linawahakikishia wakulima wa
mkonge waliojisajili ndani ya Ushirika kupitia (AMCOS) kujiunga na NHIF kupata
uhakika wa matibabu kwa kuwewezshwa na Benki ya CRDB”Alisema