Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akizungumza wakati
akifungua mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya
Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akisisitiza jambo kwa
washiriki wa mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya
Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akifafanua jambo kwa
washiriki wa mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya
Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya
Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), CPA (T) Evance
Assenga,akitoa neno la shukrani kwa Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,mara baada ya kufungua
mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume
yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia hotuba
ya Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt.
Benson Ndiege,(hayupo pichani) wakati akifungua akifafanua mafunzo kwa
kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo
Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mwezeshaji wa Mafunzo, Dkt. Ernest
Mwaswaliba kutoka Chuo Kikuu Mzumbe,akitoa mada wakati wa mafunzo kwa
kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo
Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akifatilia mada
mbalimbali wakati wa mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na wajumbe wa
Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021 jijini Dodoma.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya
Maendeleo ya Ushirika,(TCDC)Dkt. Benson Ndiege,akiwa katika picha za
pamoja na washiriki mara baada ya kufungua mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi
na wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika leo Julai 13,2021
jijini Dodoma.
……………………………………………………………….
Na Alex Sonna,Dodoma
MENEJIMENTI ya Tume ya maendeleo
imetakiwa kuzingatia mifumo ya udhibiti iliyowekwa, ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha sheria,kanuni, taratibu na miongozo inazingatiwa katika
utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
Hayo yamesemwa leo Julai 13,2021 na
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika,(TCDC) Dkt.
Benson Ndiege wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa kamati ya Ukaguzi na
wajumbe wa Menejimenti ya Tume yaliyofanyika jijini Dodoma.
Dkt.Ndiege amesema Menejimenti hiyo
inatakiwa kuzingatia mifumo ya udhibiti iliyowekwa, ikiwa ni pamoja na
kuhakikisha sheria, kanuni, taratibu na miongozo inazingatiwa katika
utekelezaji wa majukumu ya kila siku.
“Ni jukumu la Menejimenti kuhakikisha
kuwa kazi zinatekelezwa kwa kuzingatia malengo ya Tume, mipango na
mikakati ya utekelezaji wa majukumu inazingatiwa na inatekelezwa
ipasavyo na kunakuwa na matumizi mazuri ya rasilimali za Tume,”amesema
Dkt.Ndiege
Mrajisi huyo amesema Kamati ya Ukaguzi
ni chombo muhimu chenye jukumu la kusimamia kazi za ukaguzi wa ndani
kiufundi na kumshauri Afisa Masuuli kuhusu Udhibiti wa Ndani ,
Menejimenti ya Vihatarishi na Utawala Bora ili kuiwezesha Tume kufikia
malengo yake.
“Ili Kamati iweze kutekeleza majukumu
yake ipasavyo, ni muhimu Kamati ifanye kazi kwa weleledi na ufanisi.
Hivyo, mafunzo haya ninayoyazindua leo yanatarajiwa kuisaidia Kamati
kuongeza weledi na ufanisi wa utekelezaji wa majukumu yake,”amesema
Vilevile,amesema mafunzo haya
yataiwezesha Menejimenti ya Tume kuelewa majukumu ya Kamati ya Ukaguzi
na pia kujifunza wajibu wa menejimenti kuhusu utekelezaji wa ushauri na
mapendekezo yanayotolewa na ya Kamati ya Ukaguzi.
Dkt.Ndiege,amesema ili kazi ya Kamati
ya Ukaguzi ya kushauri iwe nyepesi, ni jukumu la Menejimenti ya Tume
kuhakikisaha kuwa inaweka mifumo toshelevu na imara ya udhibiti wa
ndani ili kuzuia vihatarishi vinavyoweza kusababisha Tume isifikie
malengo yake.
Mrajis huyo amesema Serikali ya Awamu
ya Sita imedhamiria kwa dhati kuendeleza na kuimarisha vyama vya
ushirika nchini ili kuleta tija kwa wanachama na hatimaye kuijenga
Tanzania yenye uchumi wa kati na wa viwanda kupitia vyama vya ushirika.
“Nina imani kuwa ushirika ukiendeshwa
na kusimamiwa vizuri unayo fursa kubwa ya kushiriki katika kujenga,
kuimarisha na kustawisha uchumi wa nchi yetu na maisha ya wananchi kwa
ujumla,”amesema Dkt.Ndiege
Mrajis huyo amewaomba wajumbe wa
Kamati na Menejimenti ya Tume kutumia fursa hiyo vizuri kujifunza
,kuuliza maswali ili kuapata ufafanuzi na kujadiliana kuhusu mada
husika ili mafunzo hayo yaweze kuleta tija katika utekelezaji wa
majukumu yao.
Naye,Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi
ya Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), CPA (T) Evance
Assenga,amesema wanachofanya katika kamati hiyo ni kupitia taarifa za
mkaguzi wa ndani na taarifa ua mkaguzi wa nje pamoja na kushauri katika
eneo la utawala bora.
“Kwa mujibu wa sheria ya fedha namba
30 inataka Taasisi kuwa na kamati ya ukaguzi,Nipende kukudhibitishia
kwamba ofisi yako tayari ina kamati ya ukaguzi na inaenda mwaka wa tatu
na inafanya vizuri.
“Kwa mujibu wa sheria inatutaka tukutane mara nne kwa mwaka na haya yote tumeweza kuyatimiza mara zote nne kwa mwaka,”amesema