Waziri
wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo akizungumza na waandishi wa
habari katika ofisi za Shirika la Viwango Tanzania (TBS) leo Jijini Dar
es Salaam.Kulia kwake ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tanzania
(TBS), Dkt.Athuman Ngenya.
(PICHA NA EMMANUEL MBATILO)
NA EMMANUEL MBATILO
Shirika
la Viwango Tanzania (TBS) wamekuwa wakijitahidi kuhakikisha bidhaa zote
zinazoingia kutoka nje na ambazo zinazalishwa hapa nchini zinakuwa na
kiwango na ubora ambao unakubalika.
Ameyasema hayo Waziri wa Viwanda na Biashara Prof.Kitila Mkumbo alipotembelea Shirika hilo leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na waandishi wa habari katika ofisi za TBS, Prof.Mkumbo amesema kuwa
wao kama Wizara wanaridhika na utendaji kazi wa shirika hilo kwani
linatekeleza majukumu yake vizuri .
“Nimewakumbusha
waongeze bidii katika kuhakikisha wanafanya kazi zao kwa ubora ule ule
lakini kwa spidi kubwa zaidi ili wafanyabiashara wanaofanya nao kazi
waweze kupewa huduma mapema iwezekanavyo”. Amesema Prof.Mkumbo.
Aidha
Prof.Mkumbo amesema kuwa TBS imekuwa haina bodi ya wakurugenzi na
majukumu yake kwa mujibu wa sheria yamekuwa yakifanywa na Katibu Mkuu wa
Viwanda na Biashara hivyo hilo jukumu lao kama serikali na amelichukua
na watalifanyia kazi mapema ili bodi ya TBS iweze kuwepo na kuendelea
kufanya kazi vizurikwa niaba ya Serikali.