Baadhi ya Vijana wa
shirika lisilo la kiserikali la Raleigh Tanzania, kupitia Mradi wa
Vijana na Mabadiliko Chanya wakifanya Usafi katika Soko la Mavunde
Chang’ombe leo April 15,2021 jijini Dodoma.
Vijana wa shirika lisilo la kiserikali
la Raleigh Tanzania, kupitia Mradi wa Vijana na Mabadiliko Chanya
wakikabidhi Vifaa vya Kutunzia Taka katika Soko la Mavunde Chang’ombe
leo April 15,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Vijana wa shirika lisilo la
kiserikali la Raleigh Tanzania, kupitia Mradi wa Vijana na Mabadiliko
Chanya wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kumaliza kufanya
Usafi katika Soko la Mavunde Chang’ombe leo April 15,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya Wanafunzi wa Sekondari ya
Dodoma wakipata elimu ya usafi kutoka katika shirika lisilo la
kiserikali la Raleigh Tanzania, kupitia Mradi wa Vijana na Mabadiliko
Chanya leo April 15,2021 jijini Dodoma.
Mratibu wa Mradi “Vijana na
mabadiliko chanya kitabia juu ya usafi” kutoka Shirika lisilo la
Kiserikali la Raleigh Tanzania Augusto Dickson,akizungumza na waandishi
wa habari mara baada ya kufanya usafi katika soko la Mavunde Chang’ombe
pamoja na kutoa elimu kwa Wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma Leo
April 15,2021 jijini Dodoma
Mmoja wa vijana wanufaika wa mafunzo
hayo Dorice Kimambo,akielezea jinsi walivyofaindika na elimu kuhusu
Usafi wa Mwili na Mazingira.
Muhamasishaji wa Masuala ya Usafi
Bw.Issa Mohamed,akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya
kufanya usafi katika soko la Mavunde Chang’ombe pamoja na kutoa elimu
kwa Wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma Leo April 15,2021 jijini
Dodoma
Na.Alex Sonna,Dodoma
Vijana
48,000 katika Mikoa Minne wanatarajia kupata elimu ya utunzaji wa
mazingira na usafi wa Mwili kupitia shirika Lisilo la Kiserikali la
Raleigh Tanzania wanaoendesha mradi wa “Vijana na mabadiliko chanya
kitabia juu ya usafi” ili kubadilisha tabia na kuepuka Magonjwa
Mbalimbali.
Hayo
yamesemwa Leo April 15,2021 na Mratibu wa mradi huo Augostino Dickson,
wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya vijana walio
katika maradi huo kufanya usafi katika soko la Mavunde Chang’ombe pamoja
na kutoa semina kwa Wanafunzi wa shule ya Sekondari Dodoma.
Bw.Dickson amesema kuwa mradi huo hivi sasa unatekelezwa katika mikoa ya Dar es saalam, Dodoma, Morogoro pamoja na Iringa.
Amesema
kuwa mradi huo umelenga katika kubadilisha mitazamo ya vijana katika
masuala ya usafi ambayo yamekuwa hayapewi kipaumbele hali inayosababisha
uchafu kuzagaa katika maeneo mengi.
“Mradi
wetu umelenga kuleta mabadiliko chanya kitabia kwa vijana na unahusisha
vijana kutoa mafunzo kwa vijana wenzao ili kupanua wigo wa uelewa juu
ya usafi na mazingira”amesema Dickson.
Aidha
amesema kuwa kupitia mradi huo walifanya tafiti kuona ni jinsi gani
wanaweza kuendesha mafunzo ya usafi kwa vijana ili kuwabadili mitazamo
yao.
“Vijana
ndiyo kundi kubwa katika taifa hivyo tuliona kuwa kwa kuwataumia wao
tutaweza kubadili mitazamo iliyopo katika jamii na kuleta mabadiliko
chanya katika suala la usafi”amesisitiza
Hata
hivyo amesema kuwa pamoja na kutoa mafunzo haya lakini pia wamekuwa
wakishirikiana katika kufanya usafi katika maeneo mbalimbali na kutoa
msaada wa vifaa vya kufanyia uasafi na kuhifadhia taka katika maeneo
kama walivyofanya ambavyo leo katika soko la Mavunde Chang’ombe na shule
ya sekondari ya Dodoma.
Kwa
upande wake Afisa afya jiji la Dodoma Abdallah Mahia amesema, kutoa
elimu katika shule kutasaidia wa wanafunzi kukua katika mazingira ya
kutambua umuhimu wa usafi ili kupepukana na magonjwa ya mlipuko.
“Sisi
kama serikali Kwa kushirikiana na Wizaraya Afya na Tamisemi, tunaungana
nanyi katika kuhamasisha uelewa wa kufanya usafi na kutunza
mazingira”amesema Mahia.
Naye
Mmoja wa vijana wanufaika wa mafunzo hayo Dorice Kimambo, amesema kuwa
wamejifunza mambo mbalimbali yanayohusu usafi na baadaye wanaenda katika
jamii kutoa elimu na kusaidia kubadili mitazamo iliyopo juu ya usafi.
“Katika
maeneo tunayokwenda kutoa elimu tumebaini bado zipo changamoto kadhaa
ikiwemo watu kuishi kwa mazoea imekuwa kikwazo kupata mabadiliko kwa
haraka, watu wengi wanadai kuwa hawana fedha za kununulia vifaa vya
kuhifadhia taka au kulipia magari ya kubeba taka”amesema Kimambo
Shirika
la Raleigh Tanzania limeendesha Zoezi la Usafi Katika Soko la Mavunde
la Chang’ombe pamoja na kutoa elimu katika Shule ya Sekondari Dodoma
ikiwa ni katika kuadhimisha kilele cha mradi huo ulioratibiwa miezi
miwili iliyopita.