Mawaziri watekeleza agizo la rais samia suluhu kikamilifu

 

Wajumbe wa kikao cha Mawaziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja naWizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas akizungumza katika kikao hicho cha kujadili hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu yaSekta hizo ya kisera, kisheria na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchini kilichofanyika jijini Dodoma leo.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas (kushoto), akifuatiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Zainab Chaula akifuatiwa na Naibu wake Dkt. Jim Yonaz katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hizo mbili cha kujadili hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo ya kisera, kisheria na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchin ikilichofanyika jijini Dodoma leo.

Katibu
Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas
(kushoto) akizungumza leo katika kikao cha Mawaziri wa Wizara hiyo na
Wizara ya Mawasiliano naTeknolojiaya Habari cha kujadili hoja zinazohusu
utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo yakisera, kisheria na kikanuni
kwenye masuala ya mawasiliano nchini kilichofanyika jijini Dodoma.Kulia
ni Katibu Mkuu waWizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt.
Zainab Chaula. Kikao hicho kimefanyika kufuatia maelekezo yaliyotolewa
hivi karibuni na Mheshimiwa SamiaSuluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania yakutaka kufanyika marekebisho ya Sheria na Kanuni
zinazosimamia Vyombo vya Habari hapa nchini hususani Televishen
Mtandao (Online TV)

 

Na John Mapepele, Dodoma

Waziri
anayesimamia Sekta ya Habari Mhe. Innocent Bashungwa na Waziri anayesimamia
Sekta ya Mawasiliano Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile na timu ya Makatibu  Wakuu na Wataalam  wa Wizara hizo  wamekaa na kujadili  hoja mbalimbali kuhusu  utekelezaji wa Sera, Sheria na Kanuni za
kisekta kufuatia  maelekezo  ya hivi karibuni ya Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Maelekezo hayo aliyatoa  
wakati wa  kuwaapisha Makatibu
Wakuu, Naibu  Makatibu  Wakuu na 
Wakuu wa Taasisi ya kufanya marekebisho ya Sheria na Kanuni  zinazosimamia Vyombo vya Habari hususan
Televisheni Mtandao (Online TV).

Majadiliano
hayo yamefanyika jijini Dodoma Aprili 14, 2021 na kutoa mapendekezo ya hatua za
kuchukuliwa kwenye hoja 13 zilizoainishwa na Wizara hizo.

Waziri wa Habari,
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa  amesema miongoni mwa  maazimio 
yaliyofikiw
a ni pamoja na kufanya  mapitio ya Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo
katika maeneo yote yenye mapungufu  ili
ziendane na  hali halisi ya sasa  na 
kuweka  mifumo rafiki ya
kushughulikia masuala  yote  yanayohusu sekta ya  Mawasiliano na Utangazaji

“Tumeagiza
Wataalam wafanye uchambuzi wa Kanuni za Maudhui Mtandaoni ili kuona kama zinaendana
na mazingira ya sasa” amesisitiza Waziri Bashungwa

Ameongeza kuwa Wizara
zimeaazimia kuja na mkakati wa kuwaelimisha 
wadau wa Sekta hizo ili kudhibiti makosa 
ya kimaudhui  yanayofanywa  na Vyombo vya Habari badala ya hali ilivyo
sasa inayotoa adhabu kali zinazojikita kwenye utozaji wa faini kubwa pamoja na
kufungiwa.

Suala lingine ambalo
limeazimiwa kufanyiwa kazi ni chaneli za bure kutoonekana kwenye visimbusi
ambavyo kimsingi zinapaswa kuonekana hata pale kifurushi kinapokuwa kimeisha
muda wake.

Kwa upande wake Waziri wa
Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya
Habari Mhe. Dkt. Faustine  Ndugulile
amesema kukua kwa teknolojia kumewezesha kukua kwa matumizi ya huduma za
mawasiliano yakiwemo ya utangazaji hivyo katika kipindi kifupi  kijacho Serikali  kupitia 
Wizara hizo mbili  itafanya  maboresho 
makubwa  kwenye kanuni husika ili
kuendana na  hali halisi ya sasa.

 

Ameongeza kuwa Serikali ilitunga Sera, Sheria, Kanuni na Miongozo
mbalimbali zikiwemo Sheria ya huduma za Habari Namba 12 ya mwaka 2016, Sera ya
Habari na Utangazaji ya mwaka 2003 na Sera ya Taifa ya TEHAMA ya mwaka 2016
ambazo pamoja na mambo mengine zinaelekeza kuweka mazingira wezeshi ya kukuza
maudhui ya ndani (Local content).

 

Naibu
Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Pauline Gekul (kushoto) akizungumza
leo katika kikao
cha Mawaziri wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari pamoja na
Wizara hiyo cha
kujadili hoja zinazohusu utekelezaji wa majukumu ya Sekta hizo ya
kisera, kisheria na kikanuni kwenye masuala ya mawasiliano nchini
kilichofanyika jijini
Dodoma, anayefuata ni Waziri wake Innocent Bashungwa akifuatiwa na
Waziri
waMawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile na kuliani
Naibu wake
Mhandisi Kundo Mathew.

Kikao hicho kimefanyika kufuatia maelekezo yaliyotolewa hivi karibuni na Mheshimiwa  SamiaSuluhu
Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania 
yakutaka kufanyika marekebisho ya Sheria na Kanuni zinazosimamia Vyombovya
Habari 
hapa nchini hususan Televishen Mtandao (Online TV)