Mkaguzi
wa TBS Bw,Sileje Lushibika akimsajili mfanyabiashara, Bw Hamza Rashid
mara baada ya kukamilisha ukaguzi katika eneo la Sokoni Wilayani
Sikonge-Tabora. Wafanyabiashara wanatakiwa wasajili majengo yao ili
wapate kibali kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za uuzaji,
usambazaji na uhifadhi wa bidhaa za chakula na vipodozi
Mkaguzi
wa TBS, Bi Zena Mushi akiendelea na zoezi la usajili kwa
wafanyabiashara wa bidhaa ya chakula na vipodozi katika kata ya Tatuo
Wilayani Sikonge- Tabora. Wafanyabiashara hao walifurahia kusogezewa
huduma hiyo na kulitaka Shirika lifanye zoezi hilo Nchi nzima
Mkaguzi
wa TBS, Bw. Sileja Lushibika akiendelea na ukaguzi wa bidhaa za chakula
na vipodozi sambamba na kukagua ukomo wake wa matumizi, pamoja na
kusajili majengo ya bidhaa hizo katika kata ya Sikonge wilayani
Sikonge-Tabora
Mkaguzi
wa TBS Bw.Sileje Lushibika akiendelea na ukaguzi wa majengo ya bidhaa
za chakula na Vipodozi katika eneo la Ipole, wilayani Sikonge ambapo
alibani uwepo wa vipodozi vilivyokatazwa ambavyo viliondolewa kwa ajili
ya kutekekezwa.
Shirika
la Viwango Tanzania limeendesha program ya kukagua bidhaa ya vyakula na
vipodozi Wilayani sikonge mkoani Tabora ili kuhakikisha wananchi
wanapata bidhaa zilizobora.
Zoezi
hilo la ukaguzi limelenga pia utoaji wa elimu kwa wafanyabiashara
kuhusu alama ya viwango kwenye bidhaa ambazo wananunua na kuuza.