Waziri kairuki apongeza juhudi za brela

Waziri
wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki akisikiliza
kwa makini jambo katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa Kiislamu katika
ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika ukumbi wa
Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.


 Msaidizi
wa Usajili Mkuu kutoka BRELA, Bw. George Chuwa akiwasilisha mada kuhusu
nafasi ya BRELA kufanikisha Tanzania ya Viwanda katika Warsha ya kwanza
ya Wanawake wa Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda
iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam


***

Waziri
wa Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji, Mhe. Angellah Kairuki amepongeza
juhudi zinazofanywa na Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA)
katika kuhamasisha urasimishaji wa Biashara.

Hayo
yamebainiswa leo alipohudhuria kama Mgeni rasmi kwa niaba ya Makamu wa
Rais Mama Samia Suluhu Hassan katika Warsha ya kwanza ya Wanawake wa
Kiislamu katika ujasiriamali na Tanzania ya viwanda iliyofanyika katika
ukumbi wa Diamond Jubilee, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza
katika Warsha hiyo Mhe. Kairuki amesema ni muhimu sana kwa
Wajasiriamali kurasimisha Biashara kwa kuwa itafungua fursa nyingi sana.

“Kurasimisha
Biashara ni muhimu sana, na ninafurahi sana kuwaona BRELA hapa, kwa
sababu, urasimishaji wa biashara unakuja na fursa mbalimbali ambazo
zinazaidia ukuaji na kuongeza kipato”.Alisema Mhe. Kairuki.

Naye
Msaidizi wa Usajili Mkuu kutoka BRELA, Bw. George Chuwa ametoa wito kwa
wanawake wote wajasiriamali kusajili majina ya Biashara zao, Alama za
Biashara au huduma, Usajili wa Kampuni na pia huduma zingine za BRELA.

“Natoa rai kwa wanawake wajasiriamali wote kutumia huduma za BRELA ambazo zote zinapatikana kwa njia ya mtandao. 

Huduma
hizo ni pamoj na Usajili waa Majina ya Biashara, Usajili wa Alama za
Biashara au Huduma, Usajili wa Kampuni, Kutoa Hataza, Kutoa Leseni za
Biashara Kundi A pamoja na kutoa Leseni za Viwanda”.

Aidha
Bw. Chuwa ameeleza kuwa ili kuweza kufungua huduma katika mfumo wa ORS
hitaji la kwanza ni kuwa na namba ya utambulisho wa Taifa kisha
kutembelea www.brela.go.tz ili kupata huduma zote.