Afisa
Udhibiti Ubora, Mhandisi Emmanuel Shilinde, akiwaonesha wanafunzi wa
shule ya msingi Chato A na B wilayani Chato, alama ya ubora ya TBS ili
waweze kuikumbuka wakati wanapotumwa kwenda kununua bidhaa
zilizozalishwa nchini. Kupata alama ya ubora kwa wajasiriamali wadogo ni
bure kabisa.
Afisa udhibiti ubora, Mhandisi
Emmanuel Shilinde (TBS) akitoa elimu ya masuala ya viwango kwa baadhi ya
wananchi wa eneo la Muganza, wilayani Chato mkoa wa Geita.
Mhandisi Emmanuel Shilinde (TBS)
akiwahamasisha wafanyabiashara wa Chato Kati – Geita kusajili madukani
ya chakula na vipodozi ili kuepuka usumbufu.
Wanafunzi wa shule ya sekondari
Chato, wilayani Chato- Geita wakisikiliza kwa makini elimu ya viwango
kutoka kwa maafisa wa TBS ili wawe mabalozi wazuri wa masuala ya viwango
katika jamii zao.
TBS imeendelea kutoa elimu ya alama
hya ubora wa bidhaa kwa wananchi Wilayani Chato ambapo wametembelea
katika shule mbalimbali za wilaya hiyo na kuwapatia elimu ili waweze
kufahamu bidhaa ambazo zimethibitishwa na shirika la hilo.
Lengo la utoaji elimu hiyo kwa
shule ni kuwafanya wanafunzi kuwa mabalozi wazuri wa shirika hilo kuhusu
alama za ubora kwenye bidhaa ili kuweza kumlinda mlaji au mtumiaji wa
bidhaa.