MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School ya
Jijini Tanga Andrew Gasper akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mashindano yaCoastal Sec City Cup ambayo yalianza
kutimua vumbi Machi 5 mwaka huu kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Galanosi
Jijini Tanga kulia ni Mwenyekiti wa Mashindano hayo Mwalimu
Yonas Mshigati na kulia ni Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Coastal
Sekondari Salimu Mwakimuna.Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Coastal
Sekondari Salimu Mwakimuna aksisitiza jambo wakati mkutano wao na waandishi wa habari kulia ni Mwenyekiti wa Mashindano hayo Mwalimu
Yonas MshigatiMwenyekiti wa Mashindano hayo Mwalimu
Yonas Mshigati akizungumzia mashindano hayo kulia ni Mwakilishi wa Kiwanda Mamujee Limited ambao ni wadhamni
Kiwanda ,Steven MalupaMwakilishi wa Kiwanda Mamujee Limited ambao ni wadhamni
Kiwanda ,Steven Malupa akielezea jambo kwenye mkutano huo
MWALIMU Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Coastal High School ya
Jijini Tanga Andrew Gasper amesema mbinu kubwa ambayo itasaidia kuiwezesha timu
ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars kufanya vizuri kimataifa ni wadau na serikali
kujikita kuweka nguvu ya pamoja kuandaa wachezaji wazawa kuanzia ngazi za chini
kupitia Mashindano ya Umitashumta,Umiseta na Vyuo Vikuu.
Mwalimu Andrew aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi
wa habari kuhusu Mashindano ya Coastal Sec City Cup ambayo yalianza
kutimua vumbi Machi 5 mwaka huu kwenye viwanja vya Shule ya Sekondari Galanosi
Jijini Tanga.
Shule ambazo zinatarajiwa kushiriki kwenye mashindano hayo
ambayo yanatazamiwa kuwa na ushindani mkubwa ni Coastal Sekondari,Galanosi
Sekondari,Chumbageni Sekondari,Old Tanga Sekondari,Usagara
Sekondari,TangaTechSekondari,Mkwakwani Sekondari,Japani Sekondari, Masechu
Sekondari na Nguvumali Sekondari.
Alisema Mashindano hayo yatakuwa chachu ya kuhakikisha
wanapatikana wachezaji wa ndani walio bora zaidi kwa ajili ya timu ya Taifa
wana vijana wa chini ya miaka U- 20,U- 17,na Taifa limekuwa likifanya vibaya
kutokana na wachezaji wa ndani kukosa misingi imara.
Alisema kwamba iwapo wachezaji ambao wanatoka kwenye
mashindano hayo wataendelezwa wanaweza kuja kuwa hazina kubwa kwa Taifa na
hivyo kuipeleka nchi kwenye mashindano makubwa Duniani na kuweza kunyakua
makombe mbalimbali
“Tukiweka nguvu kwenye ngazi za shuleni nadhani tunaweza kupata
timu ya Taifa imara ambayo inaweza kushinda timu yoyote duniani..msingi wa
Uganda kama nchi wameweza kufanya vizuri na hiyo imetokana na uwekezaji ambao
wameufanya kuanzia ngazi za chini”Alisema Mwalimu huyo.
Mwalimu huyo alisema kwamba kama wataweza kujikita kwenye
mashindano ya ngazi ya Sekondari na Msingi wanaweza kufika mbali kimataifa kama
Taifa huku akisisitiza kwamva sera ya nchi kwenye michezo lazima iweze
kutekelezwa kwa vitendo ili iweze kuwa na tija.
“Mimi nadhani sera ya nchi hata kwenye michezo lazima iweze
kutekeleza kwa vitendo na sio maneno na wawepo walimu ambao wanasimamia michezo
na hii itakuwa ni chachu kubwa kwa vijana ambao wanaweza kutumia vipaji vyao
vya soka kuweza kupata mafanikio”Alisema
Alisema iwapo wachezaji wanaoshiriki kwenye michezo
mbalimbali mashuleni watafuatiliwa na kupewa nafasi itasaidia kupunguza tabia
ya vilabu vikubwa kama Simba na Yanga kuchukua wachezaji wengi wa kimataifa na
kuwaache ya ndani.
Mwalimu huyo alisema misngi ya michezo kama Taifa ilikuwa
imebomolewa na kutokutuliwa mkazo zamani miaka 90 wakati wa Rais Mwinyi michezo
ya Umiseta ilikuwa na nguvu kubwa na ilikuwa ikizalisha wachezaji wengi sana wa
ndani ambao walikuwa na ubora wa kushindana ndani na nje.
Alisema lakini wakati alipoingia Madarakani Rais Mstaafu
Marehemu Benjamini Mkapa michezo mashuleni ilianza kudidimia na wakati wa
Jakaya ikashika kasi na hata wakati wa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa
na Rais Dkt John Magufuli michezo imeendelea kupaa juu zaidi na kurudi kwenye
wakati wake.
Awali akizungumza Mwenyekiti wa Mashindano hayo Mwalimu
Yonas Mshigati alisema kwamba lengo la mashindano hayo ni kuibua vipaji kwenye
shule za Sekondari huku akieleza michezo itakayochezwa kuwa ni mchezo wa mpira
wa miguu na pete na wanawakaribisha wadau mbalimbali ikiwemo wadhamini.
“Nitoe wito kwa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kujitokeza
kuangalia vipaji mbalimbali kwenye mashindano hayo ambavyo vinaweza kuwa chachu
kwenye timu ya Taifa za vijana na baadae kuwa hadhina kubwa ya Taifa”Alisema
Hata hivyo Mwakilishi wa Kiwanda Mamujee Limited ambao ni wadhamni
Kiwanda ,Steven Malupa allisema wao wamekwenda kudhamini mchezo wa mpira wa
miguu na pete kwa ajili ya kusapoti michezo ili kukuza vipavi kuanzia ngazi ya
chini lengo likiwa kukuza soka hapa nchini.
Kwa upande wake Mwalimu wa Michezo wa Shule ya Coastal
Sekondari Salimu Mwakimuna alisema wapo kwa ajili ya kuendesha mashindanbo hayo
akiwa kama mwakilishi kutoka shule ameisa jamii na wakuu wa shule za sekondari
watoe kipaumbele kwa michezo.
Alisema kwa sababu wanafunzi wanaposhiriki kwenye michezo taaluma
yao inapanda ikiwemo kupunguza utori wa reja reja kwa wanafunzi hatua
inayowafanya kujikuta wakipenda kuhudhuria shuleni
“Lakini hata matokeo mazuri ya kidato cha sita mwaka jana
kwa shule ya Coastal High School tulifanya vizuri vizuri kwa kushirika nafasi
ya kwanza Tanga Jiji na kimkoa nafasi ya tatu na nafasi ya 38 kitaifa na yamechagizwa na michezo ..nimpongeza mkuu wa
shulke ya Sekondari Coastal Andrew Gaspar kwa kuja na wazo hilo la kuanzisha
michezo”Alisema