Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira akizungumza wakati wa ziara hiyo |
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto wa Tanzania anayshughulikia Maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dkt John Jingu
Waziri wa Jinsia,Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Malawi,Patricia Kaliati akizungumza wakati wa ziara hiyo
Waziri wa Jinsia,Maendeleo ya
Jamii na Ustawi wa Malawi,Patricia Kaliati katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto wa Tanzania anayshughulikia Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dkt John Jingu kulia na Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za
Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira kushoto
Msajili wa NGOS wa kwanza kulia akifuatilia matukio mbalimbali wakati wa ziara hiyo
TANZANIA
imepata ugeni mkubwa kutoka nchini Malawi ambao wamekuja mkoani Dodoma nchini Tanzania
kujifunza namna ya kuendesha masuala ya Asasi za Kiraia (NGOs).
Akizungumza
wakati wa ziara ya ugeni,Mbunge wa Viti Maalumu (CCM) kupitia Kundi la Asasi za
Kiraia (NGOs) Mh.Neema Lugangira alisema ugeni huo umekuja Tanzania kujifunza
na umegongozwa na Waziri wa Malawi
anayesimamia Masuala ya Jinsia ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii.
Alisema
Waziri huyo ameongozana na Katibu Mkuu wa Ziara ya Afya na Mwenyekit wa Kamati ya
kudumu ya Bunge ambayo inasimamia masuala ya Jinsia Maendeleo ya Jamii na Ustawi
wa Jamii .
Wakiwemo
Mbunge ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo na Bodi ya NGOs ambayo inajukumu la
kuratibu shughuli zote za NGOs nchini Malawi na upande wa Tanzania uliongozwa Katibu
Mkuu wa Maendeleo ya Jamii ,Msajili wa NGos Tanzania na Mwenyekiti wa Bodi ya
NGOs Tanzania na yeye kama Mbunge wa
NGOs.
Akizungumza
wakati wa ziara hiyo Mbunge Neema alisema lengo la ugeni huo wenzao wa Malawi wapo
kwenye mchakato wa kwenda kufanyia maboresho sheria yao ya NGOs hivyo wamejaribu
kuangalia kwenye nchini za Afrika ambazo zimefanya vizuri kuratibu na kusimamia
shughuli za NGos ili kuhakikisha shughuli hizo zinapelekea maendeleo ya
wananchi.
Alisema
wananchi hao ni wale ambao wapo kwenye ngazi ya jamii walivyoratibu wakaona
Tanzania ni moja kati ya nchi ambazo zimefanya vizuri na mapinduzi makubwa
kwenye eneo hilo kuhakikisha shughuli za NGos zinasimamiwa ipaswa na zinaendana
sambamba na malengo ya Taifa na shughuli hizo zinawanufaisha wananchi wanyonge
wa Tanzania.
Awali
akizungumza wakati wa ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya Maendeleo ya
Jamii Jinsia Wazee na Watoto wa Tanzania anayshughulikia Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Dkt John Jingu alisema lengo la ziara yao ni
kujifunza kuona namna gani nzuri wao wanavyofanya katika kuratibu shughuli za
mashiriki yasiyo ya kiserikali.
Alisema
jambo kubwa nzuri ambalo wamefurahia ni namna gani ambavyo mashirika hayo
yanavyofanya kazi kwa kushirikiana na serikali na namna walivyoweka misingi ya
uwazi na uwajibika kwenye shughuli za mashirika.
Alisema
wamejifunza uzoefu wa kwao na kuna mambo wanafanya yanafafana nasi lakini jambo
moja wote tunathamini mchango wa mashirki yasiyo ya kiserikali unatoa kwenye
maeneo ya nchi wote.
Hata
hivyo alisema kwamba wanaona kuna umuhimu wa kuona mashirika hayo yafanye kazi
kwa uwazi na uwajibikaji lakini kwa kushiriki wananchi ili mchango wao uwezo
kufanikika kwenye maeneo ya nchi
Naye
kwa upande wake akizungumza wakati wa ziara hiyo, Waziri wa Jinsia,Maendeleo ya
Jamii na Ustawi wa Malawi,Patricia Kaliati akizungumza wakati wa ziara hiyoalisema wamekuja Tanzania kuangalia maendeleo walionayo
na kuona namna wanavyozingatia sheria
mbalimbali za NGOs.
Alisema
wakati wanakwenda kwenye Bunge na wataweza kufanya kazi kwa kushirikiana na
NGos kwa kuzingatia sera ya serikali inavyotaka ili kuhakikisha zinakuwa chachu
kubwa katika kupata mafanikio.
Hata
hivyo Mbunge kutoka nchini Malawi Saveoipo Kafafa alisema wamekuja kuzungumza
na serikali ya Tanzania na wabunge wa Tanzania kwa ajili ya maendeleo ya NGos
hapa Tanzania.
Alisema
nchini mwao Malawi wanafanya maboresho ya katiba ya maendeleo ya NGOs kwenye bunge
na wameendelea vizuri na mambo mengi mazuri ambayo yatakuwa chachu kuweza
kupata mafanikio .
Mwisho