Wananchi ruangwa wapokea mradi wa kilimo cha umwagiliaji wenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni moja

 

Kulia ni Mhandisi Senzia Maeda Mkurugenzi wa Idara ya Miundombinu kutoka
Tume ya Taifa ya Umwagiliagi akionesha Hati ya kukamilika kwa kazi ya
Ujenzi wa Mradi wa Nanganga kwa Uongozi wa Halmashauri ya Ruangwa,
wajumbe na baadi ya wananchi hawapo katika picha, kushoto ni Bw.
Ramadhan Mwitage mwakilishi kutoka kampuni ya Haricom International Ldt
ya Dar es Salaam Iliyofanya kazi ya ujenzi.
Picha ikionesha banio ni moja ya miundombinu katika skimu ya Kilimo cha  Umwagiliaji Nanganga.kulia Bw. Nuru Chande Makamo mwenyekiti wa kamati ya wananchi ya ujenzi
wa mradi kutoka kijiji cha Nanganga akionesha Hati ya kukamilika kwa
mradi, kushoto ni Bw. Saidi Nchia mwenyekiti wa kamati hiyo.
Picha ikionesha mfereji mkuu unaochukua maji kutoka kwenye chanzo cha maji cha mto Lukuledi na kupeleka mashambani


 Na; Mwandishi Wetu–Ruangwa


Wananchi
wa Kijiji cha Nanganga kilichopokatika kata ya Nanganga Wilayani Ruanga
MkoaniLindi, wamepokeamradiwakilimo cha Umwagiliaji, wenye thamani ya
kaisi cha fedha zaidi ya shilingi Bilioni Moja, Uliojengwa na Serikali
ya Awamu ya tano,kupitia Wizara ya Kilimo chini ya usimamizi wa Tume ya
Taifa ya Umwagiliaji kushirikiana na Halmashauri ya Ruangwa na fedha za
ufadhili kutoka Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA).

Akizungumza
kwa niaba ya wananchi wa kijiji hicho baada ya makabidhiano ya mradi
huo, Diwani wa kata hiyo Shabani Kambona alisema wamepokea mradi huo
wenye jumla ya hekta 300 za umwagiliaji ambapo ujenzi wa mradi huo kwa
awamu hii utawezesha hekta 120 kumwagiliwa .

 “Ninaishukuru
Serikali yetu pendwa kwa kuleta mradi huu na ninaimani kubwa sana kwa
wana Ruangwa kuwa sasa ni wakati wa wao kujikita zaidi katika kilimo
biashara na kuweza kupata chakula kutoka hapa hapa Raungwa bila kuagiza
nje ya Mkoa wetu, na kuongeza pato la taifa na pato la mwananchi
mmojamoja.” Alisema

Aliendelea kusema kuwa Skimu hiyo itaweza
kuwasaidia wananchi Wilayani humo kulima mazao ya chakula na mboga
mboga na kuwa na uhakika wa chakula.

Kwa upande Mwingine
pamoja na kupokea mradi huo, Diwani kambona aliiomba Serikali kumalizia
kusakafia mfereji wa upili wenye urefu wa mita elfu mbili (2000) ili
kupunguza upotevu wa maji kwenye mifereji pamoja na kuchimba mitaro nane
(8) yakutolea maji mashambani.

Mradi wa Nanganga ni kati ya
Miradi kumi na sita (16) ya SSIDP iii (Small Scale Irrigation
Development Project) ambapo kwa Mkoa wa Lindi imetekelezeka miradi
mitatu ambayo ni wa skimu ya umwagiliaji Kinyope, Nanganga na Ngongowele
Wilayani Newala