Watoto 8,082,838 kupatiwa chanjo ya surua-rubella

Waziri Ummy Mwalimu akihutubia wakazi wa Morogogo(hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa kampeni shirikishi ya chanjo


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Lowata Olesanare akiongea na wananchi walofika kiwanjani hapo 
Waziri.Ummy Mwalimu akiongea na mmoja wa mzazi ambaye alipeleka watoto wake mapacha kupatiwa chanjo kwenye uzinduzi huoMwakilishi Mkazi wa Shirika la Afya Duniani(WHO) nchini Tanzania Dkt.Tigest Mengestu akizungumza kwenye uzinduzi huo.

*******************
Na. Catherine Sungura-Morogoro
Inakadiriwa  watoto wapatao 
8,028,838 wenye umri wa miezi tisa hadi umri wa chini ya miaka mitano
(miezi 59) wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya Surua-Rubella kwenye kampeni
shirikishi  ya chanjo itakayotolewa nchi nzima.
 
Hayo yamesemwa leo na Waziri wa
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoro Ummy Mwalimu wakati
akizindua kampeni hiyo iliyofanyika  kitaifa mkoani hapa.
 
“Kampeni hii inaanza leo na
itamalizika tarehe 21 mwezi huu na itatolewa bila malipo tanzania bara
na itaendeshwa katika vituo vya kutolea huduma za afya na vituo maalam
vitakavyoundwa na kubainishwa na halmashauri katika kipindi hiki ili
kusogeza huduma karibu na walengwa”. Alisema Waziri Ummy Mwalimu.
 
Aidha, kwa upande wa kuzuia
ugonjwa wa kupooza kwa watoto wenye umri wa mwaka mmoja na nusu  hadi
miaka mitatu na nusu, Waziri huyo alisema inakadiriwa kuwa watoto 
4,041,934 watapata chanjo hiyo.
 
“Lengo kuu ni kushiriki  katika
mkakati wa kitaifa wa kutokomeza ugonjwa wa surua na rubella ili
kuchangia katika kupunguza vifo vya watoto  hapa nchi,Zoezi hili la
kampeni linatarajiwa kugharimu takribani shilingi za kitanzania billion
11.9 sawa na dola za kimarekani milioni 4.59”.
 
Hata hivyo alisema kuwa chanjo 
hupunguza gharama kubwa  ambazo familia na taifa kwa ujumla  lingetumia
katika kutibu magonjwa  yanayozuilika kwa chanjo“kuna faida kubwa
katika  uchumi wa taifa tunapowekeza kwenye chanjo,kwani imethibitishwa
kwamba kila dola moja unawekeza kwenye chanjo unapata  faida ya dola
kumi na sita”.
 
Naye Mwakili Mkazi wa Shirika la
Afya Duniani (WHO) Dkt. Tigest Mengestu alisema kuwa Tanzania inatoa
chanjo hii kwa asilimia 95 na hivyo kampeni hii inasaidia kuimarisha 
afya za watoto nchini na kuwakinga na magonjwa yanayozuilika kwa chanjo.