Jaji mruma amesema wananchi hawajua haki ni kitu gani

 


IMG_9648
JAJI Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga,Amir Mruma akizungumza wkati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo

IMG_9595
Naibu katib u Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo

IMG_9637
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shgella akizungumza wakati wa ufunguzi wa maadhimisho hayo

_MG_9614AMINA SAIDI,TANGA

JAJI
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Tanga,Amir Mruma amesema wananchi
hawajui haki ni kitu gani  anapaswa kuambiwa na polisi kabla ya
kukamatwa na kwamba nguvu ya ziada itatakiwa kutumika ikiwa mkamatwaji
anakataa kwenda kuripoti kituo cha polisi.

Mruma
ametoa kauli hiyo akimwakilisha Jaji kiongozi Dk Elieza Fleshi katika
maadhimisho ya wiki ya msaada wa kisheria ambayo kitaifa yanafanyika
jijini Tanga.

Jaji
Mruma alisema kuwa wananchi pia hawajui haki ya kujua ni muda gani
anapaswa kukaa kituo cha polisi kabla ya kufikishwa mahakamani kwa ajili
ya kusikiliza shauri lake.

“Baadhi
ya wananchi wanadhani kuwa kukamatwa na polisi ni shariti ,upigwe
makofi na mateke na  kurushwa kichura,jambo ambalo halipo kisheria,na
katika wiki hii wananchi wataelimishwa juu ya haki yao ya kisheria
wanapokutana na mazingira ya aina hiyo”alisema Jaji Mruma.

Kwa
upande wake Naibu katib u Mkuu Wizara ya Sheria na Katiba Amon Mpanju
aliwataka watanzania kuwa na utaratibu wa kuandika wosia wakati wakiwa
hai ili kuepusha migogoro ya kifamilia ambayo imekuwa ikiibuka mara
baada ya mzazi kufariki dunia.

“Migogoro
mingi imekuwa ikitokea mara baada ya mzazi kufariki dunia na hasa hasa
ni pale ambapo mzazi anakuwa hajaacha wosia wa aina yoyote,jambo hilo ni
muhimu sana kwa kuwa likifanyika hata baada ya mzazi kutopeza maisha
hakutakuwa na shida”alisema Amoni.

Naye
Mkuu wa Mkoa wa Tanga,Martine Shgella aliwataka wananchi kuyatumia
maadhimisho hayo kwenye kutatua migogoro ya ardhi katika maeneo yao
ikiwa ni pamoja na  kuwasikiliza wataalamu wa masuala ya kisheria  na
kupata shauri ambao utamaliza migogoro yao.

Katika
wiki nzima ya maadhimisho haya ambayo inatarajiwa kufikia
kilele  Novemba 17 mwaka huu wataalamu wa kisheria watakutana na makundi
mbalimbali ya kijamii katika mkoa wa Tanga na kutoa uelewa wa kisheria.