Shirikisho la soka duniani FIFA limetangaza viwango vipya vya soka duniani huku Belgium wakiendelea kuwa namba 1,
Kwa upande wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeendelea kubaki nafasi ya 134 kwenye viwango vya ubora vya Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) vya mwezi Oktoba 2020
Uganda imeendelea kuwa kinara kwa ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ikiwa nafasi ya 76 ikifuatiwa na Kenya iliyo nafasi ya 103
Nchi nyingine zilizo ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na nafasi zao ni Rwanda (133), Ethiopia (146), Burundi (148), Sudan Kusini (168), Djibout (185), Somalia (197) na Eritrea (205)
Kwa Afrika, vinara ni Senegal wakifuatiwa na Tunisia na nyuma yao wapo Algeria wakati wanaoshika nafasi ya nne ni Nigeria na Morocco wako nafasi ya tano
Top 20:
1 Belgium
2 France
3 Brazil
4 England
5 Portugal
6 Spain
7 Uruguay
8 Argentina
9 Croatia
10 Colombia
11 Mexico
12 Italy
13 Denmark
14 Germany
15 Netherlands
16 Switzerland
17 Chile
18 Poland
19 Sweden
20 Wales.