Ubalozi wa china waingia makubaliano ya ushirikiano na shirika la agri thamani foundation

 

BALOZI
wa China Wang Ke akiwa anasisitiza jambo kwa Mkurugenzi wa Shirika
lisilokuwa la Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira
BALOZI
China Wang Ke na Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la Agri
Thamani Foundation Neema Lugangira wakikabidhiana makubaliano ya
ushirikiano waliyoyasaini leo Octoba 14,2020
BALOZI
wa China Wang Ke na Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la Kiserikali la
Agri Thamani Foundation Neema Lugangira wakionyesha makubaliano ya
ushirikiano baina ya Ubalozi wa China na Agri Thamani
Foundation

************************************* 

UBALOZI wa China
umeingia Makubaliano ya Kushirikiana na Shirika lisilokuwa la Kiserikali
la Agri Thamani Foundation katika maeneo ya afya, elimu na kilimo kwa
wanawake na mabinti hapa nchini.
Akizungumza wakati wa
utiliaji saini makubaliano hayo yaliyofanyika Ubalozi wa Chini Jijini
Dar es Saaalm Balozi wa China nchini Wang Ke alisema ubalozi huo upo
tayari kuchangia maendeleo ya jamii kwa wanawake na mabinti kutoka
mikoani/vijijini na imekuwa ikitoa misaada mbalimbali  
Alisema kwamba Octoba
11 mwaka huu ilikuwa ni Siku ya Watoto wa Kike Duniani hivyo katika
kuenzi siku hiyo katika makubaliano yaliyosainiwa leo Ubalozi huo umetoa
msaada kwa Agri Thamani wa kununua taulo za kike kwa ajili wanafunzi wa
sekondari wa kike 1,500.
Balozi huyo alisema
taulo hizo za kike zitapelekwa kwenye Mikoa ya Kagera, Geita, Kigoma,
Tabora, Tanga, Dodoma na Lindi ambapo watoto hao wa kike watatoka kwenye
familia zenye uhitaji mkubwa zaidi na watapata msaada huu kwa kipindi
cha mwaka mzima ili masomo yao yasiathirike. 
Aidha pia balozi
alisema mkataba huu umesainiwa leo siku ya Nyerere ikiwa pia ni sehemu
ya kumuenzi maana aliwahi kusema Tanzania itapambana na adui wakubwa
watatu katika maeneo ya elimu, umaskini na afya .
“Mkataba huu ambao
Ubalozi wa China na Agri Thamani imesaini leo tarehe 14/10/2020 ni
jitihada za kuendelea kuenzi maneno ya Nyerere na kuyaishi kwa vitendo
lakini pia kudhihirisha ushirikiano mkubwa baina ya China na
Tanzania”Alisema Balozi huyo.
Awali akizungumza
wakati wa makubaliano hayo Mkurugenzi wa Shirika lisilokuwa la
Kiserikali la Agri Thamani Foundation Neema Lugangira  alianza
kumshukuru Balozi Wang Ke kwa utayari wake wa kushirikiana na Agri
Thamani huku akieleza huo ndio utakuwa mwanzo na wamejipanga
kushirikiana katika maeneo mahsusi yatakayopelekea kumuinua mwanamke
kiuchumi kwani ukimwezesha mwanamke na mtoto wa kike utakuwa umeiwezesha
jamii nzima.
Aidha alisema Shirika
hilo la Agri Thamani linatoa elimu ya Lishe kwenye Shule za Sekondari
na Masuala ya Hedhi Salama na Afya ya Binti ikiwa ni sehemu ya Lishe
Bora hivyo anaamini kuwa msaada huu wa taulo za kike kwa wanafunzi wa
sekondari 1,500 utakuwa msaada mkubwa sana kwa mabinti hawa hususan kwa
wale ambao watakuwa kwenye mwaka wa mitihani ikiwemo Kidato cha 2 na cha
4 ambao ndio walengwa. 
Hata hivyo alisema
kwamba ni matarajio yao kuwa mpango huo utakuwa endelevu ili iweze
kufikia wanafunzi wa kike wengi zaidi kwa kutumia ubunifu na teknolojia
mbalimbali kuhakikisha wanaondokana na changamoto ya kukosekana kwake.