Masta Mkuu Wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe akizungumza
na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa maadhimisho ya miaka
146 ya Posta duniani na kuweka wazi mikakati ya Shirika hilo kujikita
katika mfumo wa kidijitali ili kuongeza faida.
Masta Mkuu wa Shirika la Posta Hassan Mwang’ombe akizungumza na wateja
waliofika kupata huduma katika ofisi zao Jijini Dar es Salaam wakati wa
maadhimisho ya miaka 146 ya Posta duniani. Shirika hilo linatoa huduma
ya usafirishaji mizigo kwa nchi 192.
Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe akimsikiliza
moja ya mteja aliyefika kupata huduma katika ofisi zao Jijini Dar es
Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 146 ya Posta duniani. Shirika hilo
linatoa huduma ya usafirishaji mizigo kwa nchi 192.
Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe akielezea
ukarabati utakaoendana na mfumo wa Kidijitali unaofanywa katika ofisi za
Posta Jijini Dar es Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 146 ya Posta
duniani. Shirika hilo linatoa huduma ya usafirishaji mizigo kwa nchi
192.
Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania Hassan Mwang’ombe akiangali
utendaji kazi wa wafanyakazi wa Shirika la Posta Ofisi za Jijini Dar es
Salaam wakati wa maadhimisho ya miaka 146 ya Posta duniani. Shirika hilo
linatoa huduma ya usafirishaji mizigo kwa nchi 192.
*WAADHIMISHO YA MIAKA 146 YA POSTA
Na MwandishiWetu,Dar es Salaam
Katika
kuadhimisha miaka 146 ya Posta duniani, Shirika la Posta limewaasa
Watanzania kutumia huduma ya Posta kwa ajili ya maendeleo ya nchi
ikiwemo kutoa huduma ndani na nchi 192 duniani.
Shirika
Posta nchini limefanya maadhimisho hayo na kuweka wazi mikakati yake ya
kutumia teknolojia ya kisasa ili kuongeza ufanisi kwenye kazi zao na
kuwahudumia watanzania wote.
Akizungumza
na waandishi wa Habari Dar Es Salaam, katika maadhimisho ya miaka 146
ya posta duniani, Posta Masta Mkuu wa shirika hilo,Hassan Mwan’gombe
Shirika limeweza kupata faida kubwa na kuweza kutoa gawio la serikalini
Milioni 350 kutokana na mfumo wa kidijitali.
Mwang’ombe
amesema mfumo wa Kidijitali umeweza kuwasaidia na. kuboresha shughuli
za shirika hilo ndani na nje ya nchi na kujiinua kiuchumi na kupata
faida kubwa.
Amesema,
Shirika linafanya huduma ya kusafirisha mizigo nchi 192 ambazo
zinapata huduma hiyo na limeweza kuhakikisha mizigo ya wateja inafika
kwa usalama mkubwa na uaminifu.
Aidha,
Mwang’onde ameeleza Shirika la Posta lipo mbioni kuzindua huduma ya
Posta mkononi kama njia ya kuwarahisishia wateja wao kupata huduma
popote waliopo.
“Wateja
watajisajili kwa njia ya simu na kwa sasa hivi mteja hatajihitaji
kufuata barua yake katika sakundu la Posta bali itamfuata alipo.”
Amesema,
Posta ni zaidi ya barua kwani wanasafirisha bidhaa mbalimbali wana
magari yanayosafirisha vitu nchi nzima na pia wana mpango wa kuwa na
boti yao ili kurahisisha usafiri wa mizigo.
Akielezea
kwa kina kuhusiana na huduma ya Posta wakati wa mlipuko wa virusi vya
Corona, Mwa’gombe amesema “katika kipindi cha maambukizi ya virusi vya
COVID 19 serikali ilitupatia jukumu la kusafirisha sampuli kutoka eneo
moja hadi na tulifanya kazi hiyo kwa mafanikio makubwa sana.”
Nakuongeza kuwa Shirika hilo lilikuwa miongoni mwa kudhibiti janga hilo.
Pia
baada ya mkutano huo kulifanyika ziara fupi ya kutembelea baadhi ya
vitengo vinavyotoa huduma ya kusafirisha na kupokea mizingo ya wateja.