Acp advera azungumza kuelekea sikukuu za mwisho wa mwaka

Kamanda wa Kikosi cha Polisi
Tazara, Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Advera Bulimba akiongea leo na
abiria wanaosubiri kusafiri na treni kutokea Dar es Salaam kuelekea
Mbeya na Zambia. Kamanda Bulimba ametoa onyo kwa wahalifu wanaohujummu
miundombinu ya reli kuacha mara moja na amewaomba wananchi wanaoishi
jirani na reli kutoa taarifa wanapoona uhalifu wa kuiba mataruma ya reli
unatendeka.
KATIKA KUELEKEA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA, KAMANDA WA KIKOSI CHA POLISI TAZARA (DPC) KAMISHNA MSAIDIZI WA POLISI, ACP ADVERA BULIMBA
AMEWATAKA WANANCHI KUTOA TAARIFA ZA WAHALIFU WANAOWAIBIA ABIRIA WANAOSAFIRI NA TRENI ZA RELI YA TAZARA NA WALE WANAOHUJUMU RELI HIYO KWA KUNG’OA MATARUMA YA RELI.

KAMANDA BULIMBA AMESEMA KIKOSI CHAKE KIMEJIPANGA VIZURI KUHAKIKISHA WANALINDA MIUNDOMBINU YA RELI NA KUHAKIKISHA USALAMA WA ABIRIA WANAOSAFIRI KUPITIA RELI HIYO WANAKUA SALAMA WAKATI WOTE WA SAFARI YAO.

AMEONGEZA KUWA, WAPO BAADHI YA WATU WASIO WAAMINIFU AMBAO HUPENDA KUTUMIA KIPINDI HIKI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA KUJIPATIA KIPATO KISICHO HALALI KWA KUWAIBIA ABIRIA AMA KUHUJUMU NJIA YA RELI.

AIDHA , KAMANDA BULIMBA AMESEMA KUWA KIKOSI KIMEJIPANGA VIZURI NA TAYARI ASKARI WA INTELIJENSIA, MAKACHERO NA ASKARI WA MBWA
WAMESAMBAZWA MAENEO MBALIMBALI YA KIKOSI HICHO KUANZIA TAZARA DAR ES SALAAM HADI TUNDUMA.

AMETOA ONYO KALI WENYE TABIA ZA KIHALIFU KUACHA MARA MOJA NA ATAKAETHUBUTU KUFANYA UHALIFU WOWOTE WATAMCHUKULIA HATUA KALI
ZA KISHERIA.

ALIONGEZA KUWA TAZARA NI MOJA YA CHANZO CHA KUINGIZA MAPATO YA NCHI, NA ILI KUFIKIA MAFANIKIO HAYO, NI LAZIMA USALAMA WA MALI NA WATU
WANAOTUMIA RELI YA TAZARA UIMARISHWE NA NDI MAANA KIKOSI HICHI KIPO NA KIPO IMARA NA WATAHAKIKISHA MAPATO YANAYOTOKANA NA RELI YA
TAZARA HAYATA HUJUMIWA NA MTU YEYOTE.