NAIBU waziri wa maji Jumaa Aweso ametumbua meneja wa maji mkoa wa Iringa Mhandisi Shaban Gelen pamoja na meneja wa maji wilaya ya Mufindi mhandisi Robart Mgombela kutokana na uzembe wa ucheleweshaji wa utekelezaji wa maradi wa maji Sawala na Nyololo wilayani Mufindi pamoja na serikali kutuma pesa za utekelezaji wa miradi hiyo.
Aweso alisema kuwa wakati Rais Dkt Johm Magufuli akiwaapisha baada ya kuwateua aliwaeleza mambo mawili likiwemo la kuwa ninawateua nendeni mkafanye kazi ya kuwatumikia wananchi na msipo fanya kazi niliyowatuma nitawatumbueni hivyo kabla ya Rais hajamtumbua kwa kushindwa kuwatumikia wananchi ameona awatumbue hao wasaidizi wake kwa kukwamisha utekelezaji wa miradi ya wananchi .
Kwani alisema kuwa miradi hiyo ya maji ni miradi ya muda mwingi na ahadi ya Rais ni kuona wananchi wanapata huduma ya maji ndani ya mwezi wa nane ila watendaji hao kwa uzembe wamechelewesha ukamilishaji wa miradi hiyo na ule wa Sawala pamoja na kukamilika ila mhadisi wa wilaya alipewa fedha kwa ajili ya ukarabati wa tenki la maji ili wananchi waweze kupata maji safi na salama lakini ameshindwa kutekeleza na hadi sasa tenki hilo halina mfuniko wa kuzuia uchafuzi wa maji pamoja na fedha kuwepo .
Akizungumza jana baada ya kukagua maendeleo ya miradi hiyo ya maji katika mkoa wa Iringa Aweso alisema kuwa amefurahishwa nusu na utekelezaji wa miradi hiyo ila nusu hajafurahishwa na anaona ni lazima kuchukua hatua ya haraka ya kuwapumzisha watendaji hao wakuu wa maji katika mkoa wa Iringa na wilaya ya Mufindi ili kuwapata watu ambao watafanya kazi kulingana na matakwa ya serikali ya kuharakisha huduma ya maji kwa wananchi huku hao ambao walikuwepo katika nafasi hizo za juu watapangiwa kazi nyingine za kufanya na sio nafasi walizokuwa nazo.
” Wananchi wetu wanahitaji kuona wanapata huduma ya maji na sio kuona wanaendelea kupata maneno kutoka kwa watendaji wa serikali ila bado wataalam wamegeuka kuwa wana siasa kwa kutoa maneno zaidi badala ya vitendo hivyo nataka meneja wa maji mkoa wa Iringa atueleze lini mradi huu utakamilika na kwanini amechelewesha na kuifanya serikali kutoaminika kwa wananchi ” alisema Aweso
Kuwa serikali ya awamu ya tano chini ya Rais Dkt Magufuli ni serikali ya kazi zaidi na sio maneno hivyo hawezi kuona wataalamu hao wakiendelea kupiga maneno wakati wananchi wanakosa huduma ya maji hivyo njia sahihi ni wataalamu hao kupisha pendembe ili kuweka watendaji watakaowajibika kwa wananchi kuona wanapata huduma ya maji safi na salama .
Pamoja na kuwatumbua mameneja hao Aweso alipongeza mradi wa maji wa Ilula kuwa umetekelezwa vizuri na kuwatumia salumu mameneja wa maji wilaya na mikoa nchini kuwa katika ziara yake hiyo hatawafumbia macho na serikali hapo tayari kuadhibiwa na wananchi kwa kushindwa kutekeleza ahadi yake ya maji kuwa kabla ya wananchi hawajaiwajibisha serikali wao watakuwa wamewajibishwa .
Akizugumza kwa niba ya meneja wa maji wilaya ya Mufindi ,meneja wa mkoa wa Iringa Mhandisi Shabani pamoja na kuomba radhi wananchi kwa uzembe uliojitokeza aliomba kupewa muda hadi mwezi ujao ili mradi wa maji Nyololo uweze kukamilika pamoja na kuwa mradi huo hakuna shughuli iliyoanza kutekelezwa kama ya uchimbaji mitaro na usogezaji wa tofali pamoja na vifaa vya kuunganishia maji hayo