Balozi mdogo wa oman nchini anatarajiwa kuwa mgeni rasmi ufunguzi program maalum ya ukuzaji vipaji zanzibar.



Na Thabit Madai,Zanzibar.
BALOZI Mdogo wa Oman nchini Ahmed Hamood anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika ufunguzi wa program  maalumu ya kukuza vipaji vya vijana na watoto katika mchezo wa mpira wa kikapu (Basketball) ambapo program hiyo inatarajiwa kuzinduliwa katika kiwanja cha Mwanakwerekwe C, Mjini Unguja.
Program hiyo ya kukuza vipaji kwa vijana imeandaliwa na Taasisi ya vijana ya basketball  Zanzibar (ZYBA) na kuwashirikisha makindi mbalimbali ya watoto na vijana kwa jinsia zote lengo likiwa kuibua vipaji vipya katika mchezo huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya hiyo ya ZYBA, Azizi Salim alisema kwamba ZYBA imekuja na program mpya ambayo inalengo la kuwasaidia vijana na watoto kukuza  na kuendeleta vipaji vyao matika mchezo wa Basketball.
“Program inajulikana kama learn Basketball skills with ZYBA ambapo itazinduliwa na balozi mdogo wa Oman nchini Mhe, Ahmed Hamood ambapo itanyika katika viwanja vya Mwanakwerekwe C wilaya majini Unguja” Alisema Ahmed Salim.
Aliongeza kusema kwamba program hiyo itazinduliwa tarehe nane (08) mwezi huu sawa na siku ya jumamosi ambapo viongozi na watu wengi mashuhuri watakuwepo katika uzinduzi huo.
Mkurugenzi huyo aliongeza kufafanua kaamba baada ya uzinduzi Program  hiyo itakuwa inaendeshwa kila siku ya Jumamosi ambapo watoto na vijana wenye vipaji vya kucheza basketball  watakutanishwa na makocha na wachezaji wakubwa lengo likiwa kukuza vipaji vyao katika mchezo huo.
“Program hii sasa itakuwa kila siku ya jumamosi tutakuwa  na hawa watoto na vijana wenye vipaji kuwakutanisha na makocha pamoja wachezaji wakubwa kuwapa motisha na pamoja  na kukuza uelewa wao katika mchezo huu”alieleza Azizi Salim.
Pia Mkurugenzi huyo aliwataka wazazi,walezi na wadau wa mchezo  huo kujitokeza kwa wingi kuhudhuria program hiyo bayo ni bure ushiriki wake sambamba na kujitokeza kuungana mkono program hiyo ili kufanikisha.
“Mimi nataka kuwaambia kwamba Wazazi,Walezi na wadau kujitokeza kutuunga mkono kufanikisha program hii lakini pia kujitokeza kuja kushiriki ambapo ni bure kwa kila mtoto na kijana”alieleza Salim Aziz.
Program hiyo yenye lengo la kuvumbua na kukuza vipaji kwa vijana katika mchezo wa Basketball  ni mpya kufanyika visiwani Zanzibar.