Maelfu ya watu hispania warejea kazini tangu kuibuka kwa virusi vya corona

Maelfu
ya watu nchini Uhispania leo wameruhusiwa kurejea kazini, ikiwa ni mara
ya kwanza tangu kuibuka kwa mlipuko wa virusi vya corona, ambapo
serikali iliweka marufuku ya kufanyika shughuli za kawaida.


Jumatatu
ya Pasaka kwa taifa hilo haikuwa siku ya kitaifa ya mapunziko kwa raia
badala yake waliruhusiwa kuondoka majumbani mwao, ikiwa hatua ya
taratibu ya kuindoa marufuku iliyodumu tangu mwezi uliopita.

Kwa
mujibu wa makadirio ya vyombo vya habari, takribani 300,000 walirejea
makazini mjini Madrid. Kabla ya hatua hiyo, watu ambao ajira zao
zilionekana kuwa na ulazima kufanyika waliruhusiwa kufanya kazi.

Hata hivyo rekodi mpya ya maambukizi zinaonesha watu 3,477 wameambukizwa. Hayo ni katika kipindi cha masaa 24 yaliopita. 

Kwa
kuizingatia idadi hiyo, jumla ya maambukizi nchini humo kwa sasa
inafikia watu 169,496, ikionesha uelekeo wa kupatikana unafuu kwa taifa
hilo lilishambuliwa vikali na virusi. 

Katika
kipindi kigumu nchini Uhispania kulirekodiwa hadi maambukizi 8,000 kwa
siku. Vifo vipya kwa leo ni 517 na kufanya jumla yake kuwa 17,489.