Mkuu wa soko la madini Arusha Arbogast Mollel akiongea wakati akitoa ufafanuzi juu ya suala la kuwatoza wamachnga kiasi cha tsh.300 kwa siku |
Viongozi wa wamachinga wakimsikiliza mkuu wa wilaya ya Arusha Gabriel Daqarro akiongea nao leo na kutoa maagizo ya kutotozwa tozo picha zote na Ahmed Mahmoud Arusha |
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Mkuu wa wilaya ya Arusha amekemea vikali kuwatoza ushuru wamachinga wanaofanya biashara kwenye soko la madini na wilayani humo na kuwataka watu kufuata utaratibu na maagizo ya Serikali.
Agizo hilo amelitoa leo jijini Arusha wakati akiongea na viongozi wa wamachinga ofisini kwake na kubainisha kuwa zoezi hilo halina nafasi kwa kuwa maagizo ya Rais ni utekelezaji.
Amesema kuwa kimsingi hakutakuwa na mswalie mtume kwa yeyote anaye kiuka suala hilo kwa kuwatoza wamachinga fedha wakati Rais alisema wasibughuziwe .
“Nawaomba wamachinga kufanyakazi zenu bila hofu na Serikali yenu ipo kuhakikisha mnafikia mafanikio yenye kuendesha familia zenu bila kusukumwa Wala kutozwa hata Senti moja yeyote kwani mna vitambulisho halali mlivyopewa na mh.rais wetu”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.Maulid Madeni alimuakikishia mkuu huyo wa wilaya kulifuatilia suala hilo na kuondoa changamoto hiyo kwani risiti zinazotozwa sio za Serikali Wala halmashauri ya Jiji hilo haijui suala hilo.
Hata hivyo Mkuu wa soko la madini Arbogast Mollel alisema kuwa suala hilo ni makubaliano ya RMO na wamachinga hao kuhusu suala zima la Usafi wa vyoo na kwamba wamachinga hao walirudhia wenyewe.
Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Dkt.Madeni alimtaka Mkuu huyo wa soko la Madini kusitisha zoezi hilo la kuwatoza wamachinga hao