MKUU wa mkoa wa Iringa Ally Hapi amemaliza mgogolo kati ya makampuni ya Chai wilaya ya Mufindi na Halmashauri ya Mufindi juu ya utata uliokuwepo wa kodi ya shilingi bilioni 112 hadi bilioni 9.7 ambayo makampuni hayo yalikuwa yakivutana kutoa .
Awali makampuni hayo yaliingia kwenye mgogolo mkubwa na Halmashauri ya Mufindi baada ya kutakiwa kulipa kodi ya shilingi bilioni 112 ambayo Halmashauri ilikuwa ikidai makampuni hayo kabla ya mkuu wa mkoa kuunda tume ya kuchunguza uhalisia wa madai hayo .
Akipokea taarifa ya tume iliyoundwa kuchunguza madai hayo jana chini ya mwenyekiti wake Dkt Bahati Golyama ,mkuu wa mkoa wa Iringa alisema kuwa lengo la mkoa wa Iringa ni kuona wawekezaji wanafanya shughuli zao pasipo malalamiko wala mvutano na serikali na ndio sababu ya kuunda tume hiyo ili kumaliza mvutano uliokuwepo.
“Kufuatia mvutano huu uliokuwepo kati ya Halmashauri na wenye makampuni juu ya Kodi hiyo nililazimika kuunda tume ili kupitia madai hayo na kupitia sheria inasemaje na imeweza kufanya kazi vizuri na kubaini uhalisia wa deni ni shilingi bilioni 9.7 tofauti na ule wa awali wa bilioni 112″alisema Hapi
Kuwa Halmashauri ya Mufindi inapaswa kukaa na wawekezaji hao ili kuweza kuweka utaratibu mzuri wa kisheria utakaowezesha makampuni hayo kulipa fedha hizo .
Alisema utekelezaji wa zoezi hilo ufanyike katika hali ya amani na utulivu pasipo kuingia kwenye mvutano tena tena .
Alisema kuwa deni lililobainishwa na kamati iliyoundwa linapaswa kujadiliwa na Halmashauri na wadai ili kuona namna ambavyo wawekezaji hao watakavyo lipa deni hilo .
Hata hivyo alisema kuwa suala hilo lifanyike kwa kuzhirikisha mamlaka mbali mbali kama Ofisi ya Rais Tamisemi,TRA na mamlaka nyingine kwani kwa upande wake kama mkuu wa mkoa hana mamlaka ya kufuta deni hilo .
“sheria zinaelekeza wazi namna ya kufuata katika kulipa deni ama nani anaweza kufuta deni ila mkuu wa mkoa ,mkurugenzi hana mamlaka ya kufuta deni la serikali hivyo majadiliano yafanyike kwa amani na utulivu kwa pande zote mbili “
Pia alisema amemwelekeza katibu tawala wa mkoa kama mkoa uanze kufanya taratibu za mawasiliano na taasisi na ofisi mbali mbali kama ofisi ya waziri mkuu ,kilimo ,wizara ya fedha na nyingine ili kujadili suala hilo .
Pia alisema iwapo kuna mazungumzo mazuri yatafikiwa na wadau wa chai na Halmashauri basi kuingizwa kwenye sheria ili yaweze kufanyika kisheria zaidi tofauti na ilivyokuwa awali .
Mkuu huyo wa mkoa alisema kamati aliyoiunda imefanya kazi nzuri sana na hakujawa na malalamiko yoyote jambo ambalo limeweza kurejesha amani kati ya serikali na wadau wa chai .
Alisema kuwa moja kati mgogolo mkubwa uliokuwepo kati ya wawekezaji hao wa chai kampuni ya Uniliver ,Kisigo Tea Company na Mufindi Tea Company