Katibu wa ccm jamhuri mbaroni akituhumiwa kwa ubakaji

Na Ahmed Mahmoud Arusha

Katibu
wa CCM Tawi la Jamhuri kata ya Daraja mbili jijini Arusha,Aron Sanare
Kivuyo anashikiliwa na jeshi la Polisi Jijini hapa kwa kosa la kumbaka
na kumpatia ujauzito mwanafunzi wa kituo cha Compassion Mwenye umri wa
miaka 15 baada ya kumrubuni kwa fedha na mahitaji mbalimbali aliyokuwa
akimpatia

Aroni
Mwenye umri wa miaka 56 mkazi mtaa wa Sanare,Daraja mbili anadaiwa
kumpachika ujauzito mwanafunzi huyo  baada ya kumrubuni kwa kumpatia
fedha na mahitaji mengine mbalimbali na baadae alimwomba fadhila ya
ngono jambo ambalo alifanikisha adhima yake.
Diwani
wa kata ya daraja mbili Prosper Msofe amethibitisha kukamatwa na
kushikiliwa kwa kiongozi huyo wa ccm katika kituo cha polisi jijini hapa
na kueleza kuwa wao kama viongozi wanalaani vitendo vya ubakaji na
kulitaka jeshi la polisi kufanya uchunguzi ili kubaini ukweli wa tukio
hilo na sheria ichukue mkondo wake.
Akizungumzia
sakata hilo mratibu w

a kituo cha Student Center (P.A.G )kilichopo Unga
LTD jijini hapa, chenye ushirika na shirika la Compassion
Tanzania,mratibu wa kituo hicho,Yona Kaaya amesema kuwa walifanikiwa
kugundua ujauzito wa mwanafunzi huyo Mara baada ya kuona mabadiliko ya
kiafya.

Amesema
kuwa mwanafunzi huyo ambaye jina linahifadhiwa amekuwa akiishi na mlezi
wake katika mtaa wa Sanare na kusoma masomo mbalimbali katika kituo
hicho lakini juzi jumatatu alipelekwa kupimwa ujauzito katika hospital
ya Mount Meru na kugundulika kuwa anaujauzito na kumtaja katibu huyo wa
ccm kuwa ndiye mhusika Mkuu wa kupachika mimba watoto wadogo
Kwa
upande wake baba mlezi wa msichana huyo Boniface Mbwambo amesema kuwa
amekuwa akiishi na msichana huyo ambaye ni mtoto wa shemeji yake na
kwamba tukio la kubakwa na kupewa ujauzito limemshitua sana.
“Nimegundua
kuwa mtoto anaujauzito kutoka kwa wadhamini wake wanaomsomesha hapo
Compassion Mimi kama mzazi wake mlezi nimesikitishwa sana ukizingatia
aliyempa huo ujauzito ni kama babu yake ” Amesema Mbwambo.
Mkuu
wa wilaya ya Arusha ,Gabriel Gadarro amekuwa akiionya jamii kuacha
kuficha matukio hayo na kupatana kutumia mila na desturi na kueleza kuwa
serikali ya wilaya kwa kushirikiana na vyombo vya dola imeandaa mkakati
wa kuhakikisha matukio ya namna hiyo yanafiklchuliwa na kufikishwa
kwenye vyombo vya sheria.