Mahakama kuharakisha usikilizaji wa mashauri-arusha


 Gwaride
maalum lililoandaliwa na Jeshi la polisi kikosi cha kutuliza ghasia
(FFU) Kwaajili ya maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini katika
viwanja vya Mahakama ya mwanzo Arusha Mjini



 Naibu
Msajili Mfawidhi wa Mahakama kuu Arusha Sekela Mwaiseje akizungumza
katika siku ya Maaadhimisho ya siku ya sheria Mahakama ya Mwanzo Arusha
Mjini
SP Mikidadi Galilima – Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha akitoa salamu kwa  Mhe.Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna kushoto kwake ni Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana
Mhe.Jaji Mfawidhi
wa Mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna kushoto kwake ji mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo wakiwa katika Maadhimisho ya siku ya
sheria nchini katika Mahakama ya Mwanzo Arusha Mjini.
Kutoka
kushoto ni Mhe.Pamela Meena Hakimu Mahakama ya hakimu mkazi akiwa na
wenzake katika kilele cha maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria
nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Mahakama ya Mwanzo Arusha Mjini
Baadhi
ya Mhakimu wakiwa katika siku ya kilele cha maadhimisho ya siku ya
sheria nchini yaliyofanyika katika Mahakama ya mwanzo Arusha Mjini leo

Na Vero Ignatus, Arusha
Maadhimisho
ya kilele cha siku ya sheria nchini yamefanyika leo katika viwanja vya
Mahakama ya mwanzo Mjini Arusha ambapo madhumuni yake ni kuashiria
kuanza rasmi kwa shughuli za Mahakama,sambamba na kuelimisha jamii kwa
kuzingatia mada na iliyotolewa kwa mwaka husika

Akizungumza katika Maadhimisho hayo Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna 
alisema kuwa kazi kuu ya na wajibu wa msingi wa Mahakama ni kutoaji
haki kwa watu wote ambapo suala hilo siyo mambo ya Kisheria peke yake
bali ni suala la Kikatiba.
Mhe.Mzuna alisema
Mahakama inatazamiwa kuharakisha usikilizaji wa migogoro inayohusiana
na wawekezaji na ya kibiashara ili hatima yake ifahamike mapema
iwezekananyo na hivyo kuruhusu shughuli nyingine za kimaendeleo na
ukuaji wa uchumi kuendana sawa na dira ya serikali.
“Hivyo
basi serikali imejitahidi kurekebisha mfumo wa uchumi kulingana na
mazingira ya uchumi wa soko na utandawazi ikiwemo kuweka mazingira ya
kuwavutia wawekezaji mbalimbali vilevile mahakama inatakiwa iende
sambamba na mabadiliko hayo ambayo yanagusa eneo muhimu la utoaji haki
Aidha
alisisitiza kuwa Mahakama imeweka utaratibu wa kuhakikisha kuwa
mashauri hayachukui muda mrefu wala kuahairishwa pasipokuwa na sababu za
msingi ambapo katika Mahakama za mwanzo mashauri hayapaswi kukaa zaidi
ya miezi sita, wakati katika  Mahakama
za Hakimu Mkazi wa wilaya mashauri hupaswa kuchukua muda wa miezi kumi
na mbili kukamilika na kwa upande wa Mahakama Kuu shauri halitakiwi
kukaa si zaidi ya miaka miwili.
”Kuthibitisha
hili kwa mahakama Kuu Arusha mwaka juzi (2018)Mashauri yaliyomalizika
yalitumia wastani wa siku 347 kwa mwaka 2019 ni wastani wa siku 397kwa
muda wa miaka hiyo miwili wastani wake ni siku 374 sawa na mwaka mmoja
na mwezi mmoja (1.022185)’’Alisema
  Nae Mkuu wa Mashtaka mkoa wa Arusha Abdallah Chavula  mfumo
huru na madhubuti wa haki jinai katika ukuaji wa uchumi ni kuongeza
usalama wawananchi na kupunguza uhalifu sambamba na kupunguza gharama za
kiuchumi kwa serikali kutotumia uhalifu na kupunguza gharama kwa
serikali kutotumia fedha na rasilimali katika kulinda jamii na mali zao
dhidi ya vitendo vya kihalifu
Chavula alisema
kuwa matunda ya mfumo huo ni uwepo wa amani na utulivu katika jamii
hivyo shughuli za uwekezaji na biashara kuweza kufanyika kwa wepesi na
mchango wawaendesha mashtaka katika kuhakikisha kunakuwa na mazingira
wezeshi ya uwekezaji na biashara ili kusimamia na kuratibu kwa weledi
shughuli za upelelezi,kuakikisha mashtaka yanayofunguliwa mahakamani ni
yale ya yenye ushahidi madhubuti na kuendesha mashauri ya jinai bila
ubaguzi wala upendeleo  
Nae Naibu Msajili Mfawidhi wa Mahakama kuu Arusha Sekela Mwaiseje alisema
kuwa katika wiki ya Sheria Mahakama na wadau wametoa elimu ya sheria
sehemu mbalimbali ikiwemo Mrisho Gambo sekondari,Muungano ,Ilboru,Chuo
cha kilimo na mifugo Tengeru Chuo cha Ufundi Arusha pia elimu hiyo
imetolewa katika vyombo mbalimbali vya habari mkoani hapa
Elimu
hiyo iliyotolewa na mahakama imewafikia wastani wa wananchi 2565 ambapo
hesabu hiyo haijajumuisha wananchi mbalimbali ambao walisikiliza
kupittia vyombo vya habari
 SP Mikidadi Galilima – Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia Mkoa wa Arusha akimuongoza mgeni rasmi kukagua gwaride   Mhe.Jaji Mfawidhi wa Mahakama kuu kanda ya Arusha Moses Gunga Mzuna akiongozana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Jonathan Shana