Latra:ukikutwa huna leseni ya usafirishaji sheria itakushughulikia

Huu ni muonekano wa  Stendi kuu mkoa wa Arusha. Picha na Vero Ignatus)


Na.Vero Ignatus,Arusha

Mamlaka
ya Udhibiti Usafiri Ardhini mkoa wa Arusha (LATRA)inaenaendelea na
ukaguzi maalum wa magari ya abiria na malori ya kusafirsha mizigo ambayo
hayana leseni na kuyachukula hatua za kisheria.

Akizungumza kuhusiana na zoezi hilo Afisa Mfawidhi wa mkoa wa Arusha Leyla Daffa amesema
kuwa Zoezi hilo lililoanza jumanne ya wiki iliyopita katika maene
tofautitofauti ya Jiji la Arusha pamoja na wilaya zake ambapo wameweza
kukamata magari yenye makosa mbalimbali ikiwemo makosa ya kutokuwa na
leseni.

LATRA
ilifanya ukaguzi katika wilaya ya Longido na Arusha mjini katika stendi
kuu ya mabasi,Stendi ya Kilombero,Samunge na stendi ndogo  daladala
ambapo kwa(W) Arusha mjini wamekamata daladala 10 (W)Longido malori 7 na
mabasi 3 ambapo wamewachukulia hatua za kisheria ikiwemo kulipishwa
faini

Daffa alisema
magari mengi yaliyokamatwa yameadhibiwa kwa kulipa kiasi cha shilingi
laki mbili na nusu kwa kila ambaye alikamatwa kwa kutokuwa na leseni ya
LATRA kama sheria inavyoelekeza

Aidha
zoezi hilo ni endelevu kwa maeneo mengineyo haswa katika wilaya za
pembezoni katika mkoa wa Arusha zilizobakia ambazo ni
Monduli,Karatu,Arumeru

Ametoa
wito kwa wasafirishaji wote kuhakikisha kuwa wanaenda kufanya maombi ya
leseni mapema iwezekanavyo punde tu wanapobaini leseni zao zinakaribia
kwisha kwani wasipofanya hivyo Mamlaka hiyo itakamata magari hayo na
hatua nyingine za kisheria zitafuata ikiwemo kulipa faini ama kupelekwa
Mahakamani

Madereva
 wanaotumia barabara ambazo zipo katikati ya makazi ya watu LATRA
imewataka kuacha tabia hiyo mara moja kwani atakaye kamatwa akifanya
vitendo hivyo vya kukaidi na uvunjifu wa sheria  hatua kali za kinidhamu
zitachukuliwa dhidi yake

Aidha
Mamlaka ya Udhibiti Ardhini LATRA kwa mujibu wa kifungu cha 5(1)(b)cha
sheria ya LATRA namba 3 ya mwaka 2019 kutoa na kusimamia leseni za
usafirishajibabiria na mizigo ardhini ni jukumu la LATRA

Hivyo
Mamlaka hiyo imeweka utaratibu wa kutoa leseni katika ofisi za Mikoa
yote Tanzania bara hivyo mtu yeyote atakayesafirisha abiria bila leseni
ya Mamlaka husika atakuwa amevunja sheria ya LATRA kifungu cha 5 (1)(b)
na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake