Mbunge ataka wabakaji wahasiwe….serikali yagoma

Na.Faustine Gimu Galafoni,Dodoma.

Serikali imesema haiwezi kuongeza adhabu kali kwa wabakaji  zikiwemo adhabu za kuhasiwa  kwani zilizopo ni kali na zinatosha.


Hayo
yamesemwa leo Feb.4.2020  jijini Dodoma na Waziri wa katiba na sheria 
Balozi.Dkt.Augustne Mahiga wakati akijibu swali la  nyongeza la mbunge
wa viti Maalum [CCM]Mhe.Zainab Katimba aliyehoji kutokana na vitendo vya
ukatili dhidi ya mtoto wa kike hususan ubakaji kuendelea kuripotiwa
mara kwa mara ,je,serikali haioni namna ya kuongeza adhabu kali dhidi ya
watu wanaofanya vitendo hivyo.

Akijibu 
swali hilo,Waziri wa Katiba na Sheria ,Balozi.Dkt.Augustine Mahiga
amesema adhabu zilizopo kwa sasa ni kali kwani mtu aliyefanya kosa la
ubakaji ni miaka 30 mpaka wengine wanafia magerezani.

Akilitolea
ufafanuzi zaidi   juu ya suala hilo,Mwanasheria  mkuu wa Serikali
Dkt.Adelardus  Kilangi amesema pendekezo la kuhasiwa litapekekea kuvunja
katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania  katika ibara  ya 13,ibara
ndogo ya 6 ambapo inaeleza ni marufuku kwa mtu kuteswa,kuadhibiwa kwa
kinyama au kupewa adhabu  zinazomtesa au kumdhalilisha .

Naye
Waziri wa Afya ,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ,Mhe.Ummy
Mwalimu amesema sheria peke yake hazitoshi na kinachotakiwa ni wazazi na
walezi kutimiza wajibu katika ulinzi na malezi kwa watoto.