Tanzania mwenyeji wa maadhimisho ya miaka 40 ya umoja wa posta afrika (papu)


Wa
kwanza kulia ni Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
 Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano)kulia kwake ni Dkt. Jim
Yonazi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Mawasiliano)
Wa
kwanza kulia ni Dkt. Maria Sasabo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,
 Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Mawasiliano)kulia kwake ni Dkt. Jim
Yonazi, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano
(Sekta ya Mawasiliano)Eng. Clarence Ichwekeleza, Mkurugenzi wa
Mawasiliano, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya
Mawasiliano).
Baadhi
ya waandishi wa habari waluihudhuria semina iliyoandaliwa na PAPU
kupata uelewa namna ya Posta inavyofanya kazi na shughuli mbalimbali za
kimaendeleo
Baadhi
ya waandishi wa habari waluihudhuria semina iliyoandaliwa na PAPU
kupata uelewa namna ya Posta inavyofanya kazi na shughuli mbalimbali za
kimaendeleo
Na.Vero Ignatus,Arusha
Tanzania
inatarajiwa kuwa mwenyeji wa maadhimisho ya miaka 40 ya umoja wa Posta
Afrika PAPU ambapo yatafanyika Jijini Arusha kuanzia tarehe 17 -19 jan
2020 katika kituo cha Kimataifa cha mikutano AICC

 Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi,Uchukuzi na Mwasiliano(sekta ya Mawasiliano),Dkt Maria Sasabo aliyasema
hayo alipokuwa akizindua semina ya siku moja ya waandishi wa habari
yenye lengo ya kuwajengea uelewa katika sekta hiyo  ambapo alisema 
mkutano huo wa utahudhuriwa na  Mawaziri 45 kutoka nchi mwanachama wa
PAPU ,Mashirika ya Kimataifa Mabalozi wa nchi na wananchama

Dk
Maria aliesema kuwa Maadhimisho hayo ya miaka 40 ya Umoja wa Posta
Afrika ni chachu nzuri kwao kufanya tathmini ya walipotoka ,walipo na
wanapoelekea tangia kuanzishwa kwake mwaka 1980 .

Dkt.Sasabo ambaye alikuwa na Naibu Katibu Mkuu sekta ya Mawasiliano Dkt Jimmy Yonazi alisema
siku ya tarehe 18 januari 2020 litawekwa jiwe la msingi la ujenzi wa
jingo la ghorofa 16 la PAPU litakalogharimu shilingi biloni 33.5 ambapo
ujenzi huo ni ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na PAPU.

Aidha
alisema kuwa maadhimisho hayo yanakwenda sambamba na uhamashishaji wa
usajili wa laini za simu kwani zoezi hilo linatarajiwa kufikia tamati
January 20 mwaka huu hivyo kila mwenye simu anapaswa kusajili kabla ya
simu ambazo hazijasajiliwa kuzimwa.

Amewasihi
wananchi kuzitumia vyema siku hizo 20 alizoziongeza Mhe.Ris Dkt
Magufuli ambapo zimesalia siku chache kufikia tamati hivyo wazitumie
kwaajili ya kukamilisha usajili ili kuepuka usumbufu utakaojitokeza hapo
baadae
Ikumbukwe
kuwa wiki iliyopita Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi,na Mawasiliano Mhandisi
Isack Kamwele alikabidhiwa kiwanja cha kujenga jengo la PAPU barabara ya
Arusha –Moshi na kumtaka mkandarasi kampuni ya Beijing Construction
Engeneer kujenga Jengo hilo kabla ya muda wa miezi 30 kama mkataba
unavyosema na sio vinginevyo.

Alisema
kuwa mkandarasi anatakiwa kumaliza ndani ya muda au kabla ya muda
uliopangwa na katika eneo la ujenzi hakuna kuingia mtu yoyote bali ni
wale tu wenye kibali cha Wizara ya mambo ya Nje kwani eneo hilo ni la
Umoja wa Mataifa

Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele alikabidhiwa
kiwanja cha kujenga jengo la PAPU barabara ya Arusha –Moshi na kumtaka
mkandarasi kampuni ya Beijing Construction Engeneer kujenga Jengo hilo
kabla ya muda wa miezi 30 kama mkataba unavyosema na sio vinginevyo.
Aidha
alisema jengo hilo linajengwa baada ya Umoja huo unaoundwa na nchi
zaidi ya 45 za Afrika  kukubaliana kwa pamoja kuwa makao makuu yake
yajengwe Tanzania Jijini Arusha.

“Baada
ya makubaliano hayo Rais wa kwanza wa Tanzania marehemu Julius Nyerere
alitoa eneo hili mwaka 1980, lakini miaka imepita kwa sababu
mbalimbali, lakini Rais John Magufuli amehakikisha maono hayo lazima yatimie na sasa ujenzi unaanza tunamshukuru sana,”alisema.

Maadhimisho
ya miaka 40 ya Umoja wa posta Afrika{PAPU} yatakwenda sambamba na
kongamano la Mawaziri wa Nchi 45 wa sekta ya Mawasiliano litakalofanyika
Jijini Arusha leo lengo ni kujadili tulikotoka,tulipo na kupanga mpango
kazi wa miaka ijayo katika sekta hiyo.