Ruzuku ya tasaf yaboresha maisha ya wanakijiji wa mkwanda

1.  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akizungumza
na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa Kijiji cha Mkwanda wilayani
Tunduru akiwa katika ziara yake ya kikazi wilayani humo yenye lengo kukagua
utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.

1.  
Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Mkwanda wilayani
Tunduru, Bw. Adam S. Mboka akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mpango wa
Kunusuru Kaya Maskini kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (hayupo
pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo wilayani humo yenye lengo la
kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.
1.  
Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa
Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru, Bi. Aisha Jongo akitoa ushuhuda wa
mafanikio aliyoyapata kupitia TASAF kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika
(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya waziri huyo wilayani humo yenye
lengo kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.
1.  
Mnufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa
Kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru, Bw. Issa Shaban Mfaume akitoa ushuhuda wa
mafanikio aliyoyapata kupitia TASAF kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais,
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika
(hayupo pichani) wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo wilayani humo yenye
lengo kukagua utekelezaji wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.
1.  
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akisoma
bango linaloutambulisha Mradi wa Bwawa la Samaki unaotekelezwa na wanufaika 82
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru alipoutembelea
mradi huo kwa lengo la kujionea shughuli zinatofanywa na wanufaika hao.
1.  
Mradi wa Bwawa la Samaki unaotekelezwa na
wanufaika 82 wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini katika kijiji cha Mkwanda
wilayani Tunduru. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) ametembelea mradi
huo.

Na
James K. Mwanamyoto, Tunduru
Wanufaika
wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Mkwanda wilayani Tunduru wamekiri
kuboresha maisha yao baada ya kupokea ruzuku kupitia Mpango huo unaotekelezwa
na Serikali kwa lengo la kuzinusuru kaya maskini ambazo zinahitaji msaada wa kujikwamua
kiuchumi.
Baadhi ya wanufaika wa Mpango huo
wameeleza hayo wakati wa mkutano wa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) na
wanufaika hao, uliofanyika katika kijiji hicho wenye lengo la kubaini mafanikio
na changamoto za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

Akitoa shuhuda wakati wa
mkutano, mmoja wa wanufaika Bi. Aisha Jongo amesema TASAF imemuwezesha
kuboresha makazi yake kwa kuezeka bati kwenye nyumba yake na kujenga nyumba nyingine
ya bati.

“Awali nilikuwa nikiishi
kwenye nyumba ya nyasi, nilipoanza kupokea ruzuku nilianza kununua bati moja
moja mpaka zikatimia ishirini na kupaua nyumba yangu na kafanikiwa kujenga
nyumba nyingine ya bati”, Bi. Jongo amefafanua.

Bi. Jongo ameongeza kuwa,
kupitia TASAF ameweza kununua sola inayomuwezesha kupata umeme wa uhakika,
hivyo ameachana rasmi na matumizi ya kibatari.

Naye, Bw. Issa Shaban Mfaume
amesema yeye na wazazi wake wamenufaika na Mpango kiasi cha kuweza kujenga
nyumba wanayoishi sasa, hivyo TASAF imekuwa na manufaa kwani wanaishi kwenye
nyumba iliyoezekwa kwa bati.

Bw. Mfaume amemthibitishia Mhe.
Mkuchika kuwa, awamu ya pili ya Mpango imemuwezesha kuwa na bwawa la kufugia
samaki linalomuingizia kipato na hatimaye kuendesha maisha yake na ya familia
yake vizuri.

“Hamasa na elimu ya kuanzisha
bwawa langu la samaki nimeipata kupitia Mradi wa Bwawa la Samaki la kijiji cha
Mkwanda ambalo ni la walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini”, amesisitiza
Bw. Mfaume.

Akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst), Mhe.
George H. Mkuchika (Mb) kuzungumza na wanufaika hao, Mkuu wa Wilaya ya Tunduru
Mhe. Julius Mtatiro amewaasa wanufaika hao kubuni miradi mbalimbali
itakayowawezesha kutumia vema ruzuku wanayoipata kuondokana na umaskini.

Kwa upande wake, Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt.
(Mst), Mhe. George H. Mkuchika (Mb) amewapongeza wanufaika hao kwa kutumia vizuri
ruzuku kuboresha maisha yao, na kuwaahidi kuwa Serikali itaendelea kutoa ruzuku
kupitia Mpango huo ili kutekeleza azma ya kuzinusuru kaya maskini.

Mhe. Mkuchika amewatembelea
wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini wa kijiji cha Mkwanda wilayani
Tunduru ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezaji wa
Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini mkoani Ruvuma.