Mashambulizi ya roketi yafanywa katika kambi ya jeshi ya iraq ambayo ni makazi ya wanajeshi wa marekani

Jeshi
la Iraq limesema karibu makombora sita yamerushwa katika kambi ya
kijeshi ya Balad kaskazini mwa Mji Mkuu wa Baghdad leo na kuwajeruhi
wanajeshi wanne wa Iraq. 
Kambi
hiyo ambayo iko kilomita 80 kaskazini mwa mji huo mkuu ni makao ya
majeshi ya Marekani pia ingawa kiasi kikubwa cha wanajeshi wa Marekani
walikuwa washaondolewa na kupelekwa kwengine kutokana na mvutano
unaozidi kati ya Marekani na Iran.
 Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Mike Pompeo amesema ameghadhabishwa na ripoti za mashambulizi hayo. 
Taarifa
kutoka kwa jeshi la Iraq imesema roketi nane zimerushwa katika kambi
hiyo ya kijeshi jana na kuangukia katika njia ya ndege na lango la kambi
hiyo. 
Hakuna aliyekiri kuhusika na mashambulizi hayo kufikia sasa. Hakuna aliyeuwawa katika mashambulizi hayo.