Al shabaab waivamia tena kenya….walimu watatu wauawa

Watu
watatu wameuawa baada ya wanaoshukiwa kuwa wanamgambo wa Al Shabab
kuvamia mji wa Garisa kaskazini mwa Kenya katika mpaka wa Kenya na
Somalia.

Walimu watatu ambao si wa eneo hilo walipigwa risasi hadi kufa huku
kituo cha polisi kikichomwa moto na mfumo wa mawasiliano kuharibiwa
katika eneo la Kamuthe mapema leo asubihi.

Washambuliaji hao pia wameharibu mawasiliano kabla ya kutoroka.

Maafisa wa polisi wanafuatilia wavamizi hao huku ripoti za kiusalama
zikionyoesha kwamba wavamizi wameweka vilipuzi chini ya ardhi katika
barabara ya eneo hilo.

Kenya imekuwa katika hali ya tahadhari baada ya kupata taarifa za
kijasusi kwamba kundi la Al Shabab linapanga kufanya mashambulio zaidi.

Hili ni shambulizi ya 11 kutekelezwa na kundi la Al Shabab nchini Kenya
katika kipindi cha wiki 6. Mashambulizi 4 yakitekelezwa Garissa, 3
Wajir, 2 Mandera na 2 Lamu.