Watu 7 wakamatwa mwanza kwa kujifanya ni maofisa wa usalama wa taifa kutoka ikulu

Jeshi
la polisi mkoa wa mwanza kwa kushirikiana na vyombo vingine vya 
usalama limefanikiwa kuwakamata watu saba kwa tuhuma  za kujifanya
maofisa wa usalama wa taifa  kutoka ikulu, ambao hivi karibuni wamekua
wakiwatapeli wananchi na baadhi ya watumishi wa serikali katika jiji la
mwanza kwa kujifanya wako katika kazi maalum  na kuwajengea hofu ya
kiutendaji na kujenga mazingira ya vitendo vya rushwa suala ambalo
haliwezi kukubalika na kupewa nafasi katika jamii inayofuata mfumo wa
utawala wa sheria. 



Matukio
hayo yametokea kati ya  tarehe 27.12.2019  02.1.2020 hasa maeneo ya
nyakato wilayani nyamagana, na taarifa zilipopatikana kuwa wanatumia 
gari lenye na,T.751 BNL  aina ya toyota Ambulance  ambalo walidai ni
sehemu ya msafara wa viongozi wakuu walikamatwa na makachero na
wakaendelea kijitambulisha kuwa wao ni maofisa usalama wa taifa  toka
ikulu lakini walipohojiwa kwa kina ilibainika ni matapeli wenye lengo la
kuwababaisha watu kwa malengo binafsi.

Watuhumiwa waliokamatwa ni:-
  1. Chalanga Wiliam Chalanga, miaka 45, mkazi wa Pasiansi Mwanza na Arusha.
  2. Hamis Seleman mwalimu, miaka 25, huyu ni fundi magari ma hujifanya Bodyguard wa  Chalanga Wiliam Chalanga
  3. Philipo Petro, miaka 35, mkazi wa Usagara Misungwi  pia ni dereva wa Chalanga Wiliam Chalanga.
  4. Elia Vicent Gunda, miaka 30, anadai yeye ni mchungaji wa kanisa la EAGT  lililopo Kisesa, mkazi wa Kisesa,
  5. Hassan Mohamed Juma, miaka 29, mkazi wa Mkolani, fundi wa IT
  6. Selemani Joramu Karanga, miaka 25, anajifanya mlinzi  wa Chalanga Wiliam Chalanga anayejifanya ni afisa mkuu wa Ikulu.
  7. Michael Richard Mazige mkazi  wa Morogoro.
Pia,
amekamtwa  tapeli mwingine ambaye alikuwa akiwapigia watu simu na
kujifanya  kuwa yeye ni Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza, mtu huyu baada
ya kukamatwa amefahamika kwa jina la Ashery Justol @ Mnazi, miaka 30, 
mfipa, mkristo, mkazi wa Igoma Mwanza,  kabla ya kukamatwa alikuwa 
akiwapigia simu watu mbalimbali na kuwatumia ujumbe mfupi (sms) baadhi
ya watu huku akiwaaminisha kuwa yeye ndiye Kamanda wa polisi mkoa wa
Mwanza na kuwaeleza amepatwa na matatizo ya kijamii hivyo kuwataka
washiriki kwa kumchangia fedha au vitu  huku akidai mazingira aliyopo
hawezi kuongea ila watume pesa au watumie ujumbe mfupi (sms) kuwasiliana
nae.

Mtuhumiwa
huyu  alichukua picha ya kamanda Muliro  kwenye mtandao yenye sare za
jeshi la polisi na kuiweka kwenye profile yake ya whatsapp kisha
kuwapigia simu na kuwatumia ujumbe mfupi (sms) kwenye whatsapp. 

Askari
walifanya ufuatiliaji wa haraka baada ya kupata taarifa hizo na
kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa husika. Jeshi la polisi mkoa wa Mwanza
linaendelea kuwatahadharisha wananchi kuwa macho na makundi ya matapeli
ambao sasa wanaibuka na kutumia majina ya viongozi kutapeli watu.

 Wito
wa jeshi ni kuwa wakitilia mashaka  mtu yeyote watoe taarifa haraka
polisi ili hatua za haraka zichukuliwe. Watuhumiwa wote watafikishwa
mahakamani haraka iwezekanavyo.

Tukio la pili:-

 Mganga wa kienyeji atuhumiwa kumbaka mgonjwa wake

Jeshi
la polisi mkoa wa Mwanza limemkamata na linaendelea  kumshikilia mtu
mmoja aliyefahamika kwa jina la Hemed Jumanne, miaka 40, Muha, Muislam,
mkazi wa Sengerema, anayedaiwa kuwa mganga wa kienyeji, kwa tuhuma za
kumbaka mwanamke mmoja jina limehifadhiwa miaka 32, mchaga, mkristo,
mkazi wa Butimba. 

Tukio
hilo limetokea tarehe 04.01.2020 majira ya 07:00hrs asubuhi huko mtaa
wa Jiwe, kata ya Igogo wilaya ya Nyamagana, hii ni baada ya mhanga
kufika kwa mganga tajwa hapo juu kwa lengo la  kupata tiba ya maradhi
yanayomsumbua, ndipo mganga aliingiwa na tamaa ya kimapenzi na baadae
alimpa dawa za kumpumbaza kisha kumbaka kwa kuweka baadhi ya dawa  za
kienyeji kwenye sehemu za siri za mwanaume (mganga) na baadae kuingiza
sehemu za siri za mwanamke kama sehemu ya matibabu kitendo hiki cha
kikatili cha kubaka  hakivumiliki, ni cha kinyama na ni kosa la jinai. 

Muhalifu huyu atafikishwa mahakamani haraka iwezekanavyo. 

Mhanga ametibiwa hospitali na hali yake inaendelea vizuri. Kwani ameruhusiwa . 

Jeshi
la polisi linatoa wito kwa wananchi kujiepusha na makundi ya wahalififu
wanaotumia mwavuli wa uganga wa jadi kutapeli watu na kufanya vitendo
vingine vya kijinai