Ajali ya coaster na lori yaua watu 6 dodoma

Watu
sita wamefariki Dunia na wengine zaidi ya kumi kujeruhiwa katika ajali
iliyohusisha gari aina ya Toyota Coaster na lori eneo la Kisasa Dodoma
usiku wa kuamkia leo Dec 30,2019, Mganga Mfawidhi Hospitali ya Rufaa
Dodoma Dr.Ernest Ibenzi amethibitisha kupokea miili ya watu sita.


Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amethibitisha kutokea kwa ajali
hiyo na kusema kwamba chanzo chake ni dereva wa lori baada ya kuona
korongo kubwa katikati ya barabara, akajaribu kulikwepa.


Amesema wakati anahama kukwepa korongo hilo, tayari lile basi dogo la
abiria lilikuwa limeshafika karibu, na bodi la lori likaliangukia basi
hilo la abiria na kusababisha vifo na majeruhi.Dereva alikimbia, Polisi
wanaendelea kumsaka